MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
imewataka wananchi nchini kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mamlaka hiyo
katika kutekeleza hatua za uhamaji wa urushaji wa matangazo kutoka Analojia
kwenda Digitali.
Mwito huo ulitolewa na Afisa Uhusiano wa Tcra
Innocent Mungi wakati akizungumza na Vyombo vya Habari vya Mkoa wa Mbeya katika
Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Mkapa, kuhusu zoezi la uzimaji
wa Mitambo ya Analojia katika Mkoa wa Mbeya.
Mungi alisema zoezi la uzimaji wa mitambo ya
utangazaji wa Televisheni ya mfumo wa Anaolojia ulianza kutekelezwa Disemba 31,
Mwaka jana katika Jiji la Dar Es Salaam kutokana na makubaliano ya nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Alisema wananchi wanapaswa kutoa ushirikiano kwao
kutokana maandalizi ya kuzima mitambo hiyo katika Jiji la Mbeya kukamilika kwa
kuwashirikisha wananchi wa Vitongoji vyote ambapo mitambo hiyo itazimwa rasmi
Saa sita Usiku Aprili 30, Mwaka huu.
Afisa huyo alisema Elimu kwa umma kupitia mbinu
mbalimbali kuhusu mchakato wa kuhamia katika Teknolojia ya mfumo wa Utangazaji
wa Digitali imekuwa ikitolewa kwa kiwango cha kuridhisha.
Alisema matangazo ya Digitali ni mazuri kwa
sababu huwafikia watazamaji wengi zaidi kuliko Mfumo wa Analijia ambapo kati ya
Watazamaji wanaofikia asilimia 24 ni Asilimia 22 wanaofikiwa na matangazo hayo.
Kwa upande wake Mhandisi wa Maswala ya utangazaji
kutoka Mamlaka ya mawasiliano, Andrew Kisaka alisema katika Awamu ya kwanza ya
uzimaji wa mitambo hiyo itaishia katika Mkoa wa Mbeya.
Alisema hatua ya awamu ya pili itatangazwa
baadaye ambapo aliitaja mikoa ambayo imezimwa katika awamu ya kwanza kuwa ni
Dar Es Salaa (31/12/2012), Dodoma na Tanga(31/1/2013), Mwanza(28/2/2013), Moshi
na Arusha (31/3/2013) na Mbeya ambayo itazimwa mwishoni mwa mwezi huu.
Aliongeza kuwa baadhi ya vigezi ambavyo viliwekwa
na Serikali kabla ya kuanza kutekeleza suala hilo ni pamoja na Kuhakikisha kuwa
eneo linalozimwa lina huduma ya matangazo ya Digitali, Elimu kwa umma itolewe
kuhusu zoezi la uzimaji kabla ya utekelezaji.
Alivitaja vigezo vingine kuwa ni Kuendelea
kuonekana kwa Chaneli tano za Bure ambazo ni Tbc, Star Tv, Itv, Eatv na Capital
Televisheni, Uwepo wa Ving’amuzi vya kutosha katika eneo husika pamoja na
kupunguza makali ya bei.
|
No comments:
Post a Comment