Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, April 8, 2013

TANGAZO PROGRAMU MAALUMU YA KUWAANDAA WATAHINIWA KUFANYA/KURUDIA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE-2013/2014


CHUO KIKUU TEOFILO KISANJI

  
KURUGENZI YA ELIMU ANUAI


PROGRAMU MAALUMU YA KUWAANDAA WATAHINIWA  KUFANYA/KURUDIA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA  NNE-2013/2014


Chuo Kikuu Teofilo Kisanji (TEKU) kinakaribisha  maombi kutoka
Kwa watahiniwa wote waliomaliza Kidato cha Nne kujiunga na
program maalumu.

Lengo la programu hii maalumu ni kuwawezesha watahiniwa
wanaopenda kujiunga na kidato cha Tano pamoja na kozi
mbalimbali za cheti na stashahada kupata sifa itakazowawezesha
kuendelea na masomo kwangazi husika.

Masomo yataanza tarehe 30/4/2013 na yataendeshwa kwa muda
wa miaka miwili tu.  Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 28 /4/
2013 na usajili utafanyika tarehe 28/4/203. 
  
Masomo yatakayofundishwa ni kama ifuatavyo:

· Uraia (Civics)
· Historia (History)
· Jiografia (Geography)
· Kiswahili
· Kiingereza (English)
· Fizikia (Physics)
· Kemia (Chemistry)
· Biolojia (Biology)
· Hisabati (Basic Mathematics)
· Fasihi ya Kiingereza (Literature in English)

Sifa za Mwombaji:
Muombaji awe na namba ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne


Ada kwa mwaka ni Tsh. 430,000/=
Malipo haya yanalipwa moja kwa moja  kwenye akaunti za Chuo
Kikuu Teofilo Kisanji hayajumuishi gharama za
malazi, chakula na usafiri.

 Akaunti za Chuo ni kama ifuatavyo:

Teofilo Kisanji University
NBC   Account no. 016103001650
STANBIC Account no. 0140015028101
CBA Account no. 0300786000
CRDB account no. 01J1065895000

Fomu zinapatikana chuoni, eneo la Kitalu  T,  Mbeya mjini na vilevile mwombaji anaweza kuzipata kutoka katika Tovuti ya chuo: www.teku.ac.tz
Maombi yatumwe kwa:

Mkurugenzi,
Kurugenzi ya Elimu Anuai
Chuo Kikuu Teofilo Kisanji
Kampasi ya Zamani, Kitalu. T
S.L.P. 1104
Mbeya
TANZANIA

Simu: +2550252502682
Faksi: 2550252503721
Baruapepe: info@teku.ac.tz
Tovuti:   www.teku.ac.tz



No comments: