Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, April 9, 2013

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

RPC MBEYA KAMANDA DIWANIWILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                               KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 09:20HRS HUKO ENEO LA CHAMSALAKA – CHIMALA BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA . GARI T.627 AEA/T T346 AUE AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA NA DEREVA ABDU S/O OMARI,MIAKA 43,MBENA,MKAZI WA IRINGA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MARIAM D/O INCHAGI,MIAKA 18,MUWANJI,MKULIMA MKAZI WA CHIMALA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA CHIMALA MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

WILAYA YA RUNGWE -  AJALI YA GARI KUMGONGA MWENDESHA PIKIPIKI NA KUSABABISHA   
                                      KIFO NA MAJERUH.

MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 11:30HRS HUKO ENEO LA NUMBER ONE BARABARA YA MBEYA/TUKUYU WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.520 BDZ AINA YA TATA MALI YA KAMPUNI YA BONITE BOTTLES LTD MOSHI  LIKIENDESHWA NA DEREVA AINEA S/O ELIA @ SYANGA,MIAKA 38,MCHAGA,MKAZI WA MBEYA LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI T.451 CBV AINA YA KING AITWAE  SIKITU S/O ELIA ,MIAKA 38,MSAFWA, MKAZI WA MCHANGANI KIWIRA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO  NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE FRED S/O SIGARA,MIAKA 28,MSAFWA,MKULIMA MKAZI WA NDAGA TUKUYU AMBAYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MISHENI IGOGWE . CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA IGOGWE MISHENI . DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.


WILAYA YA MBEYA - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 08.04.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO ENEO LA UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA 1. DEBESHA S/O ABUSHA,MIAKA 23 NA 2. ADINA S/O ALABAYO,MIAKA 24 WOTE RAIA WA NCHINI ETHIOPIA WAKIWA WAMEINGIA NCHINI BILA KIBALI . MBINU NI KUSAFIRI KWA NJIA YA KIFICHO TARATIBU ZINAFANYWA ILI KUWAKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI . KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  MRAKIBU MWANDAMIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO  KWA JAMII KUENDELEA KUTOA TAARIFA KATIKA MAMLAKA HUSIKA JUU YA MTU/WATU WANAOWATILIA SHAKA IKIWEMO WAGENI KUTOKA NJE YA NCHI ILI HATUA  ZA KISHERIA DHIDI YAO ZICHUKULIWE.

                                                      [ BARAKAEL MASAKI - SSP ]
   KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: