BAADHI YA VIONGO ZI WA WAKIHOJIWA NA WAANDISHI WA HABARI
WASANII wa Filamu Mkoani Mbeya
wameaswa kufanya kazi kwa ushirikiano na kwa kuaminiana ili kuifanya kazi zao
kujulikana kitaifa na kupata masoko mengi ikiwa ni pamoja na kujiongezea
kipato.
Mwito huo ulitolewa na Mwenyekiti
wa Muda wa Shirikisho la Filamu Mkoa wa Mbeya, Samwel Mwamboma ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Kituo cha kusambazia Filamu cha Sam Video Centre cha Jijini Mbeya
Mwamboma alisema Mkoa wa Mbeya
unawasanii wengi sana na wazuri tofauti na Dar Es Salaam lakini wameshindwa
kujulikana kutokana na kukosa ushirikiano na uaminifu unaosababishwa na
ubinafsi ndiyo unaosababisha kutofanikiwa wala kujulikana kwa wasanii
licha ya kushiriki katika Filamu nyingi.
“ Wasanii mkiwaamini
watayarishaji wa Filamu, Wasambazaji, Waongozaji, Wapiga Picha na Waandaaji
kazi zetu zitafika mbali sana lakini mkiwa wabinafsi hatutaendelea kabisa”
Aliosema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kuwa Lengo la Kuanzisha
Shirikisho la wacheza Filamu Mkoa wa Mbeya ni kuleta Umoja ili kazi za Wasanii
wa Mkoa wa Mbeya zijulikane na kupendwa na watazamaji ili Wasanii wakubwa
kutoka Dar Es Salaamu watamani kufanya kazi nao na siyo Wasanii wa Mbeya
kutamani kuigiza na Wasanii wakubwa.
Kwa Upande Katibu wa Muda wa
Shirikisho hilo Sadi Mwang’onda alisema kuwa moja ya vitu vinavyosababisha kazi
za wasanii wa Mkoa wa Mbeya kuonekana kutokuwa na ubora ni kutokana na kila mtu
kufanya kazi kivyake bila ushirikiano ambapo Watayarishaji, Wasambazaji, Wapiga
picha na wadau kutokuwa na umoja.
Aliongeza kuwa Wasanii wa Mkoa wa
Mbeya wanakutana na Changamoto nyingi ambazo ni ukosefu wa Mitaji hivyo
kuwaomba Wakazi wa Mkoa wa Mbeya wenye mitaji kuwekeza katika Soko la Filamu
ambapo aliongeza kuwa kama wasanii wako tayari kuhakikisha Mwekezaji ananufaika
na hajutii kuwekeza kwenye Filamu za Wasanii wa Mkoa wa Mbeya.
Aliitaja Changamoto Nyingine kuwa
ni kukosekana kwa Elimu miongoni mwa Wasanii ambapo wengi wao wamekosa elimu ya
kawaida ya darasani ili hali wengine kutokuwa na ufahamu juu ya kitu
wanachokifanyia maigizo, kutokana na hilo Katibu huyo amewakikishia Wasanii
kuwa baada ya Shirikisho hilo kutulia atawatafutia Semina na Mafunzo ili wapate
mwanga kuhusu Filamu.
Katibu huyo alizitaja changamoto
zingine kuwa ni pamoja na Wasanii kutofanya utafiti kuhusu kile anachotaka
kukiigiza jambo ambalo linasababisha kazi nyingi kuonekana kama
zinafanana,ukosefu wa matangazo na wasanii wenyewe kutojiamini kutokana na kazi
wanazozifanya hivyo kuonekana ni wababaishaji tu.
Mbali na hayo Mwang’onda
aliwasihi Wasanii waliojitokeza katika Mkutano huo uliohudhuriwa na Wasanii
zaidi ya 50 kutoka Ndani ya Jiji la Mbeya, Wadau wa Filamu pamoja na Wanahabari
kuwa Wasanii wanatakiwa kuishi maisha ya Heshima kama wanavyoigiza kutokana na
Jamii kuiamini sana kazi za sanaa.
Aidha Katibu huyo alisema ili
Shirikisho lao liweze kuimarika na kuendelea watakuwa wakifanya mikutano ya
mara kwa mara na kuwataka Wasanii hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kukutana
kila wanapopata nafasi na sio kubaguana.
|
No comments:
Post a Comment