Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, April 10, 2013

Serikali Mkoani Mbeya imetajwa kuwa nyuma katika kuhamasisha wananchi kupenda zaidi kuutangaza na kuuweka Mkoa huo kuwa ni Mkoa wa Kiutalii licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii huku ukiabinishwa kujikita zaidi katika biashara.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamle
Mwenyekiti wa Chama Cha Wafanyabiashara, viwanda na Kilimo, (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Julius Kaijage akisisitiza jambo wakati wa semina hiyo ya utalii 


Mwenyekiti wa mahotel mkoa wa Mbeya Jeremia Mahenge akichangia mada katika semina hiyo


Serikali Mkoani Mbeya imetajwa kuwa nyuma katika kuhamasisha wananchi kupenda zaidi kuutangaza na kuuweka Mkoa huo kuwa ni Mkoa wa Kiutalii licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii huku ukiabinishwa kujikita zaidi katika biashara.

 Hayo yamebainishwa katika kikao cha Kamati ya Utalii Mkoa wa Mbeya kilichoketi  katika ukumbi wa hospitali ya Mkoa wa Mbeya, ambapo mbali na hilo kamati hiyo imejiwekea mikakati ya kuhakikisha inawashawishi wakazi wa Mkoa huu kuwavutia ili kuupenda na kuutangaza utalii wa ndani.

Wakichangia hoja mbalimbali wajumbe wa kamati hiyo ya utalii, walisema kuwa Mkoa wa Mbeya licha ya kuwa na vivutio vingi vya kiutalii ambavyo vikiboreshwa na kupendwa na wakazi wa Mkoa huo wanaweza kupata fedha nyingi kutoka kwa watalii, lakini wakazi wa Mbeya pamoja Serikali yake imejikita zaidi katika masuala ya Kibiashara.

Mjumbe wa kamati hiyo  ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Rosemary Senyamle, alisema kuwa  Mkoa wa Mbeya unakosa fursa ya kujitangaza kupitia utalii uliopo kutokana na wakazi wengi kuelekeza zaidi mawazo yao katika biashara huku akibainisha kwamba Mkoa umejitangaza na umefanikiwa kuwa ni moja ya mikoa ya kibiashara.

“Mbeya imejiweka zaidi kibiashara kuliko utalii na hili nadhani linachangiwa na Serikali ya Mkoa kutoweka kipaumbele zaidi kuutangaza Mkoa katika sekta ya utalii licha ya kuwa na utajiri mwingi wa vivutio vya kiutalii ambavyo tukiungana kwa pamoja  tunaweza kusonga mbele zaidi ya hapa tulipo kwa kuwa na wageni wengi wanaokuja kwa kibiashara na  kiutalii pia,” alisema Mjumbe huyo.

Aidha, wajumbe hao walisema pamoja na kuwa Mkoa wa Mbeya kuwa na sura ya kibiashara  kwa kipindi kirefu, wakazi wa Mbeya na Viongozi wao wanawajibu wa kuubadili na kuwa sura ya Kiutalii zaidi ili kuendelea kuwavutia wageni wengi kuja ndani ya Mkoa wa Mbeya.

Hata hivyo, kamati hiyo inakusudia  kukuza utalii wa ndani  kwa kuwapa watu wa Mbeya habari sahihi kwa  vipeperushi  na matangazo  yatakayohusiana na  utalii ili waelewe na kuanza kufanya shughuli za  kiutalii sehemu mbalimbali zenye vivutio.

No comments: