MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amewataka viongozi wa
dini kutoa ushauri kwa waumini pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha kujihusisha
na vitendo vya mauji ya kikatili vivavyo endelea kujitokeza siku hadi siku
katika maeneo yote Mkoani hapa yanayo hatarisha uvunjifu wa amani na kuliletea
sifa mbaya jiji la Mbeya,
Kandoro aliyasema hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya sikukuu ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo kimkoa yalifanyika Wilayani Rungwe na
kuhudhuria na viongozi mbalimbali kutoka katika Wilaya zote za Mkoa wa
Mbeya,baada ya kutokea matukio mfululizo ya mauaji ya kinyama yanayohusishwa na
imani za kishirikina,
Baada ya kutoa ushauri huo kwa viongozi wa dini,Mh,Kandoro
pia alizungumzia mfumo wa serikali mbili Serikali ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ndiyo yenye dola inayo shughulikia Utawala,Ulinzi na usalama
na masuala yote ya muungano na mambo ya Tanzania Bara yasiyo ya muungano,
Alisema kuwa kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ina mamlaka juu ya mambo yasiyo ya muungano yanayohusu Zanzibar tu kama
ilivyoainishwa katika sehemu ya kwanza ya katiba ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake,
Aliongeza kuwa Kila mmoja wetu anao wajibu wa kudumisha
umoja,mshikamano na muungano wetu kwa kuwaenzi waasisi wa Muungano wetu ambao
ni Hayati Baba wa Taifa Mwl ,Julius Nyerere pamoja na Hayati Sheikh
Abed Karume ambao walipiga vita udini,ukabila, Rushwa na aina zote za
ukiukwaji wa haki za binadamu,
‘’Ndugu zangu wana Rungwe na wana Mbeya wote tunatakiwa
tuuenzi Muungano wetu pamoja na kudumisha Amani,Utulivu,Upendo na
mshikamano miungoni mwa watanzania na majirani zetu,kupiga vita
umasikini,ujinga na maradhi,kuimarisha misingi ya Utawara bora na
Demokrasia’’,alisema Kandoro,
Pia ailiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika
shughuri mbalimbali za maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya
madarasa,nyumba za waalimu pamoja na ununuzi wa madawati ili kupunguza
changamoto katika shule zetu na vijana wetu waliopo katika shule za msingi na
sekondari waweze kusoma vizuri na kupata matokeo mazuri pindi wamalizapo
masomo yao.
Picha na Ally Kingo Rungwe
|
No comments:
Post a Comment