Mwendesha mashtaka wa Serikali Basilius Namkambe
aliaambia Mahakama hiyo Mbele ya Jaji Samweli Karua kuwa watuhumiwa hao
walitenda kosa hilo Mei 15,2011 katika Kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira
Wilayani Rungwe kinyume na kifungu cha 196(16) kilichofanyiwa marekebisho Mwaka
2002.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Hakimu
Mwakalinga ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja katika kesi hiyo akiwa na Daudi
Mwasipesya,Obote Mwanyimbili na Kelvin Maurus Myovela ambao wanatuhumiwa kumuua
John Mwankenja aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kiwira(CCM) na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Awali baada ya kupandishwa kizimbani watuhumiwa
kujibu kesi inayowakabili yenye namba 31/2012 walimkataa Wakili aliyejulikana
kwa jina moja laMwakabubu aliyekuwa ameteuliwa kwa ajili ya kuwatetea kwa madai
kuwa hawana imani naye kutokana na mwenendo wa kesi alizosimamia.
“Mtukufu Jaji kabla ya kesi yetu haijaanza kusikilizwa
tunaomba kubadilishiwa Wakili kwa sababu huyu Mwakabubu hana uwezo na tumeona
kesi ndogo tu anababaika na kesi yetu ni kubwa tunaona wazi kabisa kuwa
hataweza kututetea” alisema Mwakalinga Mshitakiwa namba moja.
Kufuatia ombi hilo Jaji Karua alikubaliana nao
ambapo alimteua Wakili mwingine ambaye ni Sambwee Shitambala ambaye walimkubali
kabla hajawaongezea wakili mwingine ili asaidiane na Shitambala ambapo alimtaja
Wakili Zakia Selemani.
Akisoma mashtaka yao Mwendesha mashtaka wa
Serikali Basilius Namkambe aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 19,
Mei 2011 majira ya jioni marehemu akiwa anatokea Mbeya mjini akirudinyumbani
kwake Kiwira Wilayani Rungwe alifika Nyumbani akiwa na gari lenye namba za
usajili T 127ACZ Nissan (Double cabin).
Namkambe aliongeza kuwa baada ya kufika nyumbani
kwake alipiga honi ya gari kwa ajili ya kuomba kufunguliwa geti la mlango
ambapo baada ya kusikia honi hiyo alitoka Mjomba wake ambaye baada ya
kumfungulia aliambiwa ashushe Kuku aliyokuwa amewabeba nyuma ya gari yake.
Alisema kabla ya mjomba wa Marehemu hajaanza
kushusha kuku kwenye gari alitokea mshitakiwa namba moja akiwa na siraha ambapo
alimwamuru asifanye lolote ndipo akaanza kufyatua risasi akimwelekezea marehemu
kisha kumuuana kutoweka kusiko julikana.
Akijibu tuhuma hizo Wakili wa Utetezi Shitambala
na Zakia walikana washtakiwa hao kuhusika na matukio hayo pamoja na baadhi ya
vielelezo vilivyotolewa na upande wa mashtaka kuthibitisha kuhusika kwa wateja
wao.
Walisema mtuhumiwa wa kwanza hakuwepo Wilayani
Rungwe siku ya tukio ambapo walisema atakuwa na mashahidi ambao watathibitisha
kwamba hakuhusika ambao waliwataja kuwa ni pamoja na yeye mwenyewe, Askari
Magereza wawili wa gereza la Tukuyu Wilayani Rungwe waliotajwa kwa jina moja
moja la Hereda na Green.
Wengine ni Padeso Mwakipesile, Aneth Siandene
Kalinga na Jumanne Mwakisole huku washtakiwa namba mbili, tatu na nne ambao
hawatakuwa na mashahidi ambapo watasimama wao wenyewe kujitetea.
Namkambe aliiambai mahakama hiyo kuwa upande wa
mashtaka utakuwa na mashahidi zaidi ya 15 ambao aliwataja kuwa ni pamoja na
Sofia Fungameza, Weston Gilbert,Magdalena Mgawe, Musa Jackson, Issa Mwaipopo,
Teresia Ludovick na Williamu Mtanga.
Wengine ni askari Polisi Mwenye namba D2385
Sajent Michael wa Tukuyu, Inspekta Isaya Bwile wa Tukuyu, David Paul kutoka
makao makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Twaha kutoka kitengo cha Upelelezi makao
makuu ya Polisi Dar Es Salaam, Haruna kutoka Polisi Tukuyu na WP3433 Agnes wa
polisi Tukuyu.
Namkambe aliwataja mashahidi wengine katika kesi
hiyo kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa upelezi (RCO) Mkoa wa Mbeya
aliyehamishiwa makao makuu SSP Anacletus Malindisa, John Mayunga na Dk. D Z
Matata kutoka ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali.
Jaji Karua aliahirisha kesi hiyo hadi hapo
itakapopangwa tena kwa ajili ya kuendelea na kuwasilikiza mashahidi kutoka
upande wa mashtaka baada ya kuambia mahakama kuwa upelelezi umekamilika na
mashahidi wote wako tayari.
Na Venance Matinya, Mbeya.
No comments:
Post a Comment