WAANDISHI WA HABARI WAKIWA OFISI YA JEM MINISTRY WAKIONGEA NA
MKURUGENZI JEREMIA MWAKANYILENGE
-->
KWAKUA MITUME WA KWELI YEYE NI MUHUDUMU WA JAMII
NA MUNGU HUYAFANYA MAMBO MAGUMU KUWA MEPESI
Hayo yasememwa na mtume JEREMIA MWAKANYILENGE wa
huduma ya Jem ministry ya jijini mbeya alipokuwa akiitambulisha huduma hiyo kwa
waandishi wa habari ofisini kwake.
Mwakanyilenge amewataka waumini kuwa makini sana
na huduma hizi zilizoshamili kuibuka kila siku kutokana na kuwepo na baadhi ya
watumishi matapeli wanaotumia jina la kristo kujinufaisha wenyewe binafsi
“Ukiona mtume huduma yake inaleta uchochezi
katika taifa hili ujue huyo si wa mungu atakuwa amejituma mwenyewe na ni
tapeli, kwani aliyetumwa na mungu kweli huyafanya yaliyo magumu kwa watu kuwa
mepesi” amesema mwakanyilenge.
Katika kikao hicho pia alipata nafasi ya
kuitambulisha rasmi hudu yake ya JEM MINISTRY kua si kanisa jipya bali ni
tasisi ya kuihudumia jamii kwa kuwapatia ajira katika idara zake za biashara
kama vile JP PRODUCTION studio inayofanya kazi za kurekodi audio cd pamoja na
video, lakini pia imeanzisha mfuko wa kustaafu wachungaji.
JP PRODUCTION imetoa ajira kwa wachungaji na
vijana mbalimbali wenye kipaji cha uimbaji kwa kujikimu na maisha yao kama
wengine, Lakini pia imekuwa ikisambaza kazi za waimbaji kwa kuwapa faida kubwa
kuliko wasamabazaji wengine.
Kwa hivi sasa JEM MINISTY
pamoja na JP PRODUCTION imeto kazi mpya ambayo ipo sokoni yenye nyimbo nane
zilizoimbwa live na mtumishi wa mungu JEREMIA MWAKANYILENGE kwa kushirikiana na
mwaimbaji wa kimataifa EFRAIM SEKELETI toka nchini zambia.
|
No comments:
Post a Comment