NDUDU WA SAMSON DANIEL ALIYOWATEKETEZA KWA MOTO 2010
Mahakama kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu kutumikia
kifungo cha miaka 35 Samsoni Daniel Mwang’ombe baada ya kupatikana na hatia ya
kuua bila kukusudia ndugu wa familia moja wapatao saba.
Akisoma mashtaka mbele ya jaji wa mahakama hiyo
Samwel Karua, Mwendesha mashtaka wa Serikali Rhoda Ngole alisema mtuhumiwa huyo
alitenda kosa hilo Juni 21, 2010 kinyume cha kifungu cha 195 (16)
kilichofanyiwa marekebisho Mwaka 2002.
Ngole aliiambia Mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa
alitenda kosa hilo mwaka huo majira ya 2:00 hadi saa 2:30 usiku ambapo alifika
nyumbani kwa baba yake akiwa na sigala mkononi huku akiivuta na baadaye
kuidondosha sigala hiyo iliyosababisha moto kuwasha nyumba.
Aliwataja walioathirika na moto uliokuwa
umewashwa kutokana na sigala aliyokuwa ameidondosha mtuhumiwa kuwa ni
Daniel Mwang’ombe, Anitha Richard, Salome Mwang’ombe,Jane Samson, Diana Samson,
Maria George na Cloud Samson.
Kutokana na kosa hilo mtuhumiwa huyo alikiri
kuhusika na kwamba aliua bila kukusudia ambapo alikiri kuwa akiwa anavuta
sigala alidondosha kipande hicho ambacho kilikuwa bado kinawaka moto.
Aidha Mwendesha huyo aliiambia mahakama hiyo kuwa
pamoja na mtuhumiwa kukiri kusababisha vifo bila kukusudia mahakama impe adhabu
kali kwa mujibu wa sheria.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo Wakili wa
upande wa utetezi Sambwee Shitambala alisema Mahakama inatakiwa kumwonea
huruma na kumpunguzia adhabu mshtakiwa kutokana nay eye kuwa miongoni mwa
wafiwa.
Alisema mshtakiwa ameondokewa na wazazi, watoto
na mke katika ajali hiyo ambapo hakuhudhuria mazishi yao pia amekaa muda mrefu
akiwa mahabusu ambapo amekaa kwa miaka mitatu na kuongeza kuwa mtuhumiwa
ni kijana ambaye ni nguvu kazi ya taifa hivyo hastahili kufungwa.
Hata hivyo kutokana na utetezi huo Jaji Karua
alisema kutokana na hali iliyojitokeza mtuhumiwa atatumikia kifungo cha miaka
mitano kwa kila tukio ambalo ni kusababisha vifo saba hivyo jumla atatumikia
miaka 35
Na Venance Matinya, Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment