SERIKALI wilayani Rungwe
imeendelea kuwashukuru wadau wa elimu kuendelea kutoa misaada mbalimbali
ili kuweza kumalizia ujenzi wa vyumba vya madasara katika shule za wilayani
hapo na kuhakikisha wanafunzi wote waliofaulu mitihani yao ya darasa la saba
mwaka jana kujiunga na kidato cha
kwanza haraka iwezekanavyo.
Kauli hiyo ya Serikali imetolewa
na Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela, mara baada ya kupokea msaada
wa mifuko 200 ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya shilingi 3.5 Milioni, kutoka
kwa kampuni ya Mohamed Enterprises Limited (Metl) yenye kiwanda cha kusindika
majani ya Chai wilani hapo amabyo alikabidhiwa jana wakati
alipotembelea kiwanda hicho kwa lengo la kujionea uzalishaji wake.
Meela alisema kuwa moja ya
matunda ya wawekezaji ndani ya wilaya hiyo ni kuona namana wanavyokuwa mstari
wa mbele katika kuisadia jamii inayowazunguka na si vinginevyo na kwamba hilo
lipo hata katika shueria za uwekezaji nchini.
Alisema kuwa juhudi zinazooneshwa
na wawekezaji wa ndani katika kuhakikisha watoto wote waliofaulu mitihani yao
ni kuendelea kujenga na kukarabati vyumba vya madarasa.
Mkuu huyo alibainisha kwamba
misaada hiyo imekuja kwa muda mwafaka kwasababu zaidi ya wanafunzi 700
waliofaulu mtihani wao wa darasa la saba mwaka jana wameshindwa kujiunga na
kidato cha kwanza wilayani hapo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa hivyo
misaada hiyo itasaidia kukamilisha ukarabati huo na kuona wanafunzi wote
wanakwenda shule.
“Niendelee tu kuwashukuru watu
muhimu kama hawa wa Kampuni ya Mohamed Enterprises kuliona kuwa wilaya yetu
tunawanafunzi zaidi ya 700 walioshindwa kujiunga na kidato cha kwanza kutokana
na upungufu wa vyumba vya madarasa,”alisema na kuongeza.
“Tunatambua kuwa licha ya
mikakati ya serikali ya kuhakikisha hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa tatu
ukarabati wa vyumba hivyo uwe umekamilika na wanafunzi wawe wameanza
masomo, makampuni ya viwanda vilivyo wilayani hapa vimejitoa kweli kutusaidia
kwa mwezi uliopita tu tumepokea mifuko 100 ya saruji kutoka kampuni moja
na nyinyi leo mnatuunga mkono kwa kutupatiwa mifuko 200 mingine kweli msaada
mkubwa sana kwetu,” alisema Meela.
Awali Meneja wa Kamupni hiyo ya
Metl, George Mwamakula, alisema kuwa wao kama wawekezaji wa ndani moja ya furaha
yao kuona wanaishi na jamii ya watu waliosoma hivyo hawataona kazi kuendelea
kusaidia jamii hiyo katika sekta ya elimu pamoja na sekta nyingine muhimu kama
vile maji, umeme, afya na barabara.
“Hata sisi tunatambua wazi kwamba
jamii isiyokuwa na elimu ya kutosha wawekezaji hawawezi kukaa kwa amani kwani
migogoro isiyokuwa lazima lazima itatokea tu lakini kama jamii hii itapatiwa
elimu ya kutosha hakutakuwa na migogoro baina ya wawekezaji na wananchi husika
kwani mgogoro wowote unajipotokeza inakuw rahisi kuutatua kwa amani zaidi,”
alisema Mwamakula.
|
No comments:
Post a Comment