Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Thursday, February 28, 2013

WAKAZI wa Mtaa wa Igodima kata ya Iganzo Jijini Mbeya waandamana kushinikiza kutekelezewa ahadi walioahidiwa na Diwani wa Kata hiyo ya kuwagawia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.

Wakazi  zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata ya Iganzo wakidai kupewa eneo la kufanyia biashara huku wakiwa na majembe wakimtaka mweshimiwa diwani wa kata hiyo awagawie eneo hilo kwani wamechoka kudaganywa mara kwa mara
Ni vurugu tupu
Diwani Uswege Furika (Chadema) kata ya iganzo akiwatuliza wakazi wake watulie ili awaeleze ukweli kilichotokea
Kiukweli mambo yote anayafahamu yulee yaani akimnyooshea afisa mtendaji wa kata hiyo kuwa anafahamu vyema juu ya kiwanja hicho cha soko 
Afisa Mtendaji wa kata Iganzo Jumapili Mwasenga  amemkana mweshimiwa diwani kuwa hana taarifa yeyote juu ya swala hilo huku akisema jamani wananchi muulizeni vizuri diwani wenu sisi tunafanya kazi kimaandishi
Wananchi wangu sasa sijui tufanyeje maana naona hili swala limekuwa gumu kwangu  itabidi nikae na uongozi wangu halafu nitawapa jibu
Mweshimiwa diwani tuna taka haki yetu 
Mweshimiwa diwani twende eneo la tukio ukatupatie maeneo yetu tuanza biashara tunaomba sana baba  huyo dada akimsihi mweshimiwa diwani
Mbona hamnielewi nimewaambia ngoja nikae naviongozi wenzangu tuwashughulikie swala lenu mweeeee
Wakazi wa Iganzo baada ya kuone hawamweliwi diwani wao wakaamua kuondoka kueleea kwenye kwenye eneo walilotakiwa kupewa ili wakajigawie wenyewe maeneo yao
Haooo wanaondoka
Mweshimiwa diwani haamini macho yake anapoona wananchi wake wanaondoka bila ya kumsikiliza
Hili ndilo eneo walilotakiwa kugawiwa sasa wananchi hao wanachagu uongozi wao wa muda ili waanza kujigawia eneo hilo
HILI NDILO ENEO WANANCHI HAWA WATAJIGAWIA WENYEWE KWA AJILI YA SOKO BAADA YA MWESHIMIWA DIWANI KUWADANGANYA


WAKAZI wa Mtaa wa Igodima kata ya Iganzo Jijini Mbeya wameandamana kushinikiza kutekelezewa ahadi walioahidiwa na Diwani wa Kata hiyo ya kuwagawia eneo kwa ajili ya kufanyia biashara.

Wakazi hao zaidi ya 50 wameandamana hadi katika Ofisi za kata na kupokelewa na uongozi wa kata hiyo akiwemo Diwani Uswege Furika (Chadema) na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Jumapili Mwasenga  huku wakiwa na majembe mikononi wakishinikiza kuanza kugawiwa eneo hilo.

Awali ilidaiwa kuwa Diwani huyo aliwaahidi wananchi hao kuwapa eneo kwa ajili ya biashara ambapo aliwaambia wananchi hao kufika eneo husika asubuhi mapema kwa ajili ya kila mtu kuoneshwa sehemu yake ambayo angefanyia biashara zake.

Aidha katika hali isiyokuwa ya kawaida Diwani huyo alipingana na wananchi hali iliyozua mzozo  mkali baina yake na wananchi ambapo alikataa kutoa ahadi hiyo lakini baada ya kubanwa sana alikubali na kudai kuwa suala hilo alilifikisha kwa Ofisa Mtendaji wa Kata.

Baada ya Ofisa mtendaji kupewa nafasi ya kulizungusuala hilo pia alipingana na Diwani huyo kwa madai kuwa ofisi yake haikuwa na taarifa juu ya ahadi hiyo hivyo alichokifanya Diwani huyo alipotosha wananchi.

Ofisa huyo Jumapili Mwasenga alisema suala la Wnanchi kudai eneo la Soko ni madai ya msingi lakini yana taratibu zake namna ya kuyapata kuongeza kuwa kama Diwani aliahidi alitakiwa kutoa taarifa Ofisini kwake ili walifanyie utaratibu.

Aliongeza kuwa pamoja na ahadi hiyo bado yeye kama Mtendaji anatekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi na siyo Chama kingine hivyo Diwani alipaswa kupeleka maombi ya wananchi kwa maandishi ili yafanyiwe kazi.

Kufuatia majibu hayo yaliyoibua hasira kali kwa wananchi ambao walianza kupiga kelele wakidai kuoneshwa eneo ili wakaanze kupanga meza tayari kwa biashara  ambapo Mtendaji huyo aliwaahidi wananchi kusubiri ili taratibu zianze kufanyika ili wapewe eneo hilo.

Wananchi hao hawakulizika na majibu ya Mtendaji huyo hali iliyopelekea kumbana Diwani wakidai kuwa hawana imani naye kwa kuwa alikurupuka kutoa ahadi huku akifahamu utaratibu unaotakiwa kufuatwa kabla ya kuanzishwa kwa soko.

Godfrey Sanga mkazi wa Mtaa wa Igodima alisema Suala la maendeleo ya kata ya Iganzo limekuwa likipigwa danadana kila siku ambapo Diwani kupitia mkutano wa chama cha Chadema uliofanyika Jumapili iliyopita aliwaahidi wananchi hao kuwa wafike kwa ajili ya kupewa maeneo hali iliwalazimu wananchi kufika eneo hilo wakiwa na majembe mikononi.

“ Wanatuona kama watoto tusiokuwa na akili huyu diwani yeye mwenyewe aliahidi kututengenezea barabara  na soko alisema lipo eneo tayari sisi tuje ili kila mtu apewe sehemu yake lakini badala yake anatugeuka” alihoji Hassan Kasangula mkazi wa mtaa wa Igodima.

Hata hivyo wananchi hao walionesha kutoridhika na kauli za viongozi hao hali iliyowalazimu kufika eneo la soko na kuchagua uongozi wa mpito na kuanza kujigawia tayari kwa kuanza biashara huku uongozi ukibaki unashangaa.

Aidha kufuatia hali hiyo Diwani huyo alimtupia lawama Mwenyekiti wa Chadema wa kata hiyo kuwa ndiye aliyetoa ahadi hiyo kwenye mkutano hali iliyosababisha yeye kulaumiwa na wananchi akihusiashwa na ahadi hiyo.

No comments: