Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa
wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale
ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Wananchi wa Mtaa wa
Ilolo Kata ya Manga Jijini humo kumfukuza mtaani hapo Mwanamke anaye fahamika
kwa jina la Zainabu Zuberi akituhumiwa kuhusika na ushirikina.
Wananchi hao ambao
awali walitaka kujichukulia hatua mkononi kwa kumpiga na kumchomea moto nyumba
yake mtuhumiwa huyo walidai kuchoshwa na maovu yanayofanywa na mwanamke huyo.
Baadhi ya matendo ya
kishirikina wanayomtuhumu mwanamke huyo kuhusika nayo ni pamoja na kujigamba
kuwamaliza wanakijiji hao kwa kuwaloga ikiwa ni pamoja na kuwaloga watoto wao
kitu ambacho wanasema kimeshatokea.
Wamedai kuwa mwanamke
huyo amekuwa akiwagusa wanawake wajawazito na mimba zao huharibika ambapo pia
wanafunzi wanaotoka katika mtaa huo wakifika Shule hushindwa kuona kabisa matukio
ambayo mwanamke huyo anahusishwa.
Walisema mwanamke huyo
anatuhumiwa kujihusisha na matukio ya kishirikina tangu ahamie mtaani hapo
takribani miaka mitatu ambapo walisema wakazi hao walimwonya mapema kuhusu
tabia hiyo baada ya kufuatilia historia ya maeneo aliyowahi kuishi.
Kwa upande wake Mume
wa Mtuhumiwa huyo Sulemani Rubea(49) amekataa mke wake kutuhumiwa kwa
ushirikina ambapo aliwatupia lawama wanakijiji kwa madai kuwa wanaendekeza
udini na kutopenda maendeleo na ndiyo maana hawawataki mtaani hapo.
Rubea ameongeza kuwa mtaani
hapo hawapendi mtu wa dini ya nyingine kujenga eneo hilo jambo ambalo
lilipingwa vikali na wananchi waliohudhuria mkutano wa hadhara uliokuwa na
lengo la kumjadili mtuhumiwa huyo.
Awali mume wa
mtuhumiwa huyo alikiri kuhama nyumba na mitaa zaidi ya kumi ambapo lisema
maeneo mengine alikuwa amejenga lakini sehemunyingine alikuwa amepanga tu
ingawa aligoma kusema sabbu inayomfanya ahame maeneo hayo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilolo Kati Ngambi Kulaba Ngambi amesema wananchi walikuwa
wakimtuhumu yeye kuwa anamlinda mwanamke huyo ili aendelee kuishi mtaani pale
ili hali wao hawamtaki mtaani hapo.
Amesema baada ya kuona
wanachi wamepagawa na kutaka kujichukulia hatua mkononi ili mlazimu kuitisha
mkutano wa hadhara ikiwa na kuitaarifu jeshi la polisi ambalo lilifika mapema
eneo la Mkutano na kwatuliza wananchi wasifanye lolote ambapo Askari hao
waliondoka na mtuhumiwa.
Aidha katika mkutano
huo wananchi hao kwa pamoja waliazimia kumhamisha Mwanamke huyo Mtaani hapo
katika mkutano ulihudhuriwa na wakazi zaidi ya 200 ambao walidai kuchoshwa na
hali hiyo.
Matukio kama hayo
yanayoashiria vitendo vya kishirikina ni pamoja na tukio la hivi karibuni la
watu wawili kuzikwa wakiwa hai wakituhumiwa kuhusika na vitendo hivyo viovu
ndani ya jamii.
Na Mbeya yetu
|
1 comment:
Mbeya ni lini tutaona habari za maendeleo na upendo, ni mauaji, uchawi,ajali. Hakika inasikitisha, Mbeya inasadikika kuwa na madhehebu mengi Tanzania lakini ndiko uchawi, mauaji na kila aina ya uovu unafanyika. Ni kitu gani ambacho wana Mbeya wanaweza kuonesha ulimwengu cha kujivunia kama si aibu tu.
Tumejaa kujisifu na kujivuna tu,tunahitaji mabadiriko, tunahitaji kumuomba Mungu abadirishe hii roho ya kutisha ya mauaji na maovu mengine.
Mimi mdau niko mbali na Mbeya lakini kila ninapofungua hii blog ninachokutana nacho mara nyingi ni matukio ya kienyeji kabisa (Barbaric).
Post a Comment