MAMLAKA ya udhibiti
wa huduma za nishati na maji(EWURA) imetoa siku 21 kwa shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO ) kuwasilisha majibu dhidi ya hoja zilizotolewa na wateja wa
shirika hilo jijini Mbeya kuhusu kubambikiwa deni la zaidi ya Sh.Mil.16 katika
nyumba za kanisa Katoliki Jimbo la Mbeya.
Katika barua
yenye kumbukumbu nambari EWURA/33/1/194/2 ya januari,4,2013 iliyoandikwa na
Mkurugenzi wa Mkuu wa Eura Tanzania,Haruna Masebu kwenda kwa mkurugenzi
mtendaji wa Tanesco Makao makuu imeliagiza shirika hilo kusitisha deni na
makato yake kuendelea kuwapatia huduma ya umeme wateja hao hadi mamlaka
itakapotoa uamuzi wa shauri hilo.
Barua hiyo yenye
kichwa cha habari Taarifa ya Malalamiko na wito wa kuleta maelezo yako dhidi ya
malalamiko ya wateja wa Tanesco Mbeya kubambikiwa deni nakala pia imesambazwa
kwa Waziri wa nishati na madini,Prof.Sospeter Muhongo (MB),Meneja wa Tanesco
Mkoa wa Mbeya na walalamikaji.
Mkurugenzi
Masebu amesema kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 5(1) cha kanuni za taratibu za
kutatua migogoro za Ewura [The energy and Water Utilities regulatory
Authority(Consumer complaints settlement procedure)
Rules,GN.No.30/2008},Tanesco inatakiwa kuwasilisha majibu dhidi ya malalamiko
yaliyotolewa na wateja wake katika gazeti moja la kila siku(siyo Jambo leo) la
Jumatano,Januari,2,2012.
Inahitimisha
sehemu ya maagizo ya Mkurugenzi wa Ewura kuwa Tanesco izingatie kuwa kushindwa
kuwasilisha utetezi wake ndani ya muda uliotajwa kutaiondolea haki yake ya
kusikilizwa na Ewura itaendelea kufanya maamuzi katika shauri hilo kwa
kuzingatia hoja za upande mmoja kwa mujibu wa kanuni zilizotajwa na kwamba
majibu ya Tanesco kwa ewura walalamikaji wapewe nakala.
Wakizungumzia
barua hiyo baadhi ya walalamikaji hao ambao ni wapangaji katika nyumba za
Kanisa Katoliki jimbo la Mbeya zilizonunuliwa kutoka shirila la reli Tanzania
(TRC) Aidary Khalfan na Mohamed Tamimu wamesema kuwa tangu wamepokea barua hiyo
bado Tanesco hawajatekeleza agizo la kuwarejeshea huduma ya umeme na nakala ya
barua ya kujibu hoja Ewura ambapo ilipaswa na wao wamapate nakala lakini
hawajapelekewa(walalamikaji).
Wametoa wito kwa
Viongozi wa ngazi za juu wa shirika hilo kuwa makini na baadhi ya watumishi wao
wa ngazi za chini kwani wanaweza kulipeleka Shirika kubaya kutokana na
kufanyakazi kwa maslahi yao binafsi, kulifanya shirika kama mali yao wakati ni
la watanzania na hivyo kuweza kulitia hasara kubwa.
Hata hivyo
wamesema licha ya kupata majibu ya kejeli na kukatishwa kabisa tamaa na
wafanyakazi wa Tanesco kuhusiana na madai yao hawakukata tamaa na kuamua
kufikisha sauti hiyo kupitia vyombo vya habar.
Aidhai wametoa
wito kwa watanzania kuvitumia vyombo vya habari pindi wanapoona wananyanyasika
ili wahusika waweze kuwasaidia kuliko kukaa kimya na kuendelea kuteseka.
Meneja wa Shirika la Tanesco,Mkoa wa Mbeya
enginia ,John Bandiya alipotakiwa kutoa ufafanuzi kuhusu kukaidi agizo la
Ewura,amesema barua ilielekezwa kwa mkubwa wake ambaye Mkurugenzi mtendaji
makao makuu hivyo hana lolote la kusema.
|
No comments:
Post a Comment