Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 4, 2012

WANANCHI SONGWE MBEYA WAANDAMANA KUTAKA MATUTA





 SISI NI WANAFUNZI, WAZAZI NA WENZETU WAMEPOTEZA MAISHA HAPA KWA KUGONGWA INGAWA KUNA PUNDA MILIA LAKINI MADEREVA HAWAJALI KAULI ILE YA KIBURI SI MAUNGWANA

 JAMANI SISI NI VIONGOZI WA WILAYA HII, TUNAOMBA MTUSIKILIZE


 NAITWA SIMON MKINA KAIMU MENEJA WA TANROAD MBEYA, KWA LEO HAIWEZEKANI LAKINI TUTAJENGA MATUTA



BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Songwe wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani Mbeya wameandamana tangu asubuhi kwa ajili ya kuishinikiza Serikali kuweka matuta eneo hilo baada ya kutokea ajali za mara kwa mara eneo hilo.

Wamesema kuwa hatua hiyo wameifikia baada ya kushuhudia ajali mbaya jana ambapo aligongwa mtoto Ezekiel Mwaula wa shule ya Msingi Saruji.

Uongozi wa wilaya ya Mbeya pamoja na Tanroad mkoa wa Mbeya wakiongozwa na Injinia Simon Mkina wamefika kuwaomba wananchi kutuliza hasira, hatimaye wananchi wamekubali kwa kuchagua viongozi watano ii kufuatilia 
utekelezaji.

Kwa hisani ya Kalulunga

No comments: