Standi kuu ya mbalizi
BAADHI ya waandishi wa habari mkoani Mbeya wamesema kuwa
watahusika kwa asilimia 100 katika kuungana na vijana wa Mji mdogo wa Mbalizi
wilaya ya Mbeya Vijijini mkoani humo kufanya usafi wa kufagia na kuzibua mitaro
unaotarajia kufanyika kesho (Jumatano).
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa
Nsungwe uliopo Mbaizi, mratibu wa Vijana wazalendo wa mji wa Mbalizi Gordon
Kalulunga, alisema kuwa baadhi ya waandishi wa vyombo mbalimbali waliopo mkoani
Mbeya wamefurahishwa na wazo la vijana hao hivyo wamemwakikishia kuwa nao
wataungana nao.
Kalulunga alisema kuwa baadhi ya waandishi hao wanatoka kwenye
Mgazeti ya Tanzania Daima, Mwananchi, Sauti huru, Jambo Leo na Habari leo,
Televisheni ya Taifa TBC1, Star TV na redio Mbeya yetu blog zilizopo mkoani Mbeya.
Alisema anawashukuru waandishi hao na wanataaluma wengine ambao
watashiriki katika tukio hilo la kihistoria na kwamba vijana wa Mbalizi
wanaomba kupitia kwao vijana wengine poote Tanzania wafanye hivyo katika maeneo
yao ili kuifanya Tanzania salama.
‘’Mbali na waandishi wa habari na vijana wengine ambao watatoka
nje ya wilaya yetu ya Mbeya Vijijini, tumekutana na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa
wilaya yetu Emmanuel Mwaigugu ambaye ni mratibu wa kitengo cha kinga na tiba
ameonyesha jinsi gani Serikali imethamini wazo hili na kuwa tayari kushirikiana
nasi pale tunapokwama’’ alisema Kalulunga.
Sanjari na hayo alisema baada ya kufanya usafi huo katika eneo
la Tarafani watafanya tathimini na kujiwekea malengo ya kufanya usafi kama huo
katika eneo linguine.
Naye Kijana Raphael Kajange alisema kuwa hapo baadae anaamini
kila mwananchi atakuwa balozi wa kulinda na kutunza mazingira ya mji wa Mbalizi
na kila kaya.
No comments:
Post a Comment