Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 4, 2012

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) YATOA ZAIDI YA SHILINGI MILION 15 KWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA AJILI YA KUBORESHA MFUMO MPYA WA UTOAJI HUDUMA ZA MATIBABU KWA NJIA YA MAWASILIANO (TELE MEDICINE)

Meneja wa TCRA Kanda ya Nyanda za Juu kusini Deograsias Moyo kwa niaba ya mkurugenzi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania akimkabidhi hundi ya zaidi ya sh milioni 15 mkurugenzi wa hospitali ya rufaa Mbeya eliuter Samnkey 

ZAIDI  ya shilingi million 15 zimetolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzanzania (TCRA)  nyanda za juu kusini   ajiri ya  kuboresha mfumo  mpya wa utoaji  huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano (TELE MEDICINE) ili kupunguza vifo na  gharama za usafiri kwa wagonjwa.



 Mhandisi  na kaimu meneja wa mamlaka ya mawasiliano ya simu (TTCL) George Mtikila akipokea hundi hiyo  kwa mkurugenzi wa hospitali ya rufaa dr Eliuter Samnkey kwa ajili ya kuleta vifaa hivyo na kufunga katika hospitali hiyo ya rufaa Mbeya

ZAIDI  ya shilingi million 15 zimetolewa na mamlaka ya mawasiliano Tanzanzania (TCRA)  nyanda za juu kusini   ajiri ya  kuboresha mfumo  mpya wa utoaji  huduma za matibabu kwa njia ya mawasiliano (TELE MEDICINE) ili kupunguza vifo na  gharama za usafiri kwa wagonjwa.

Mkurugenzi  Mkuu wa Hosptal ya Rufaa jijini Mbeya Eleuter Samky alishukuru mamlaka hiyo na kueleza kuwa mfumo huo utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa   kupunguza  vifo na jamii kupatiwa huduma bora licha kuwepo na changamoto ya upungufu wa madaktari bingwa.

“Mfumo huu utatusaidia sana na kuweza kuokoa maisha ya watanzania kwani kutakuwepo na mawasiliano mazuri na kuelimishana njia mbalimbali za kuweza kutoa matibabu kwa wagonjwa wetu hususan magonjwa ya watoto  na mgonjwa sugu yaliyoshindikana kutibika“Alisema.


Mhandisi  na kaimu meneja wa shirika la simu (TTCL) George Mtikila alisema kuwa  mkataba huo  wameingia na mamlaka ya mawasiliano (TCRA) utaanza kutumika kwa wakati na kwamba  lengo kuu ni kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa  katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi.

Jengo la TTCL Mbeya
Mitambo ya kisasa ya mkonge wa taifa
Hudi iliyokabidhiwa leo
Moja ya wataalam wa mkonge wa taifa Humphrey Ngowi akiwaeleza waandishi wa habari jinsi mtambo huo unavyofanya kazi

No comments: