Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, December 4, 2012

Ujue utamaduni wa kabila la wasafwa wa jijini Mbeya


Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kulia) akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi (kushoto) ambaye ni Mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya moja ya nyumba ya kale iliyokuwa inatumiwa na kabila la wasafwa ambalo ni kabila maarufu mkoani humo. Mponzi ameamua kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ambacho kitatunza kumbukumbu za utamaduni na mila zote ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Msafwa wa Mwasanga jijini Mbeya Ibrahim Saimon akipuliza pembe ya Mnyama aina ya Tandala “Ndundwe” iliyokuwa inapingwa wakati wa sherehe za kumaliza msiba “matanga” za kabila la wasafwa. Sosteli Mponzi ameamua kujitolea kujenga kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila hilo ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakimuangalia Mary John akisaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe aina ya “Lwala” wakati walipotembelea ili kujionea ujenzi wa kituo cha utamaduni wa kabila lao kinachojengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi. Baadhi ya wasafwa waishio maeneo ya vijijini bado wanasaga unga wa ulezi kwa kutumia jiwe hilo kwa ajili ya kutengenezea pombe.
Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Sosteli Mponzi (kushoto) akimuonyesha Victoria Zitta Mnyanyi ambaye ni mshauri wa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya mti wa asili aina ya msulusulu ambao wazee wa kabila la wasafwa walikuwa wakiutumia kwa ajili ya kutibu mifugo. Mponzi ameamua kujitolea kujenga kituo cha utamaduni wa kabila hilo ili kumbukumbu zisiweze kupotea kwani hivi sasa kutokana na utandawazi makabila mengi yamekuwa yakipoteza utamaduni wao.
Baadhi ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakicheza ngoma aina ya Mbeta ya kabila hilo ambayo inachezwa wakati wa kumaliza msiba “Mwengulo” kama walivyokutwa na mpiga picha wetu hivi karibuni alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila la wasafwa. Ujenzi wa kituo hicho unajengwa kwa kujitolea na Sosteli Mponzi ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Mkazi wa Mwasanga jijini Mbeya Juma Changa akionyesha jinsi wazee wa zamani walivyokuwa wakichonga mpini wa jembe kwa kutuma teso “menzo” wakati mpiga picha wetu alipotembelea kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila la wasafwa huku Said Mbata (kulia), Victoria Zitta Mnyanyi (katikatia) na Sosteli Mponzi (kushoto) wakimuangalia. Ujenzi wa kituo hicho unajengwa kwa kujitolea na Mponzi ili kizazi kijacho kiweze kufahamu mambo yaliyofanywa na mababu zao.
Baadhi ya wasafwa wa Mwasanga jijini Mbeya wakimwonyesha mpiga picha wetu jinsi wazee wa zamani wa kabila hilo walivyokuwa wanakunywa pombe aina ya Kimpumu wakati alipotembelea kujionea ujenzi wa kituo cha kutunza utamaduni na mila za kabila hilo.Kutokana na kuenea kwa magonjwa mbalimbali ya kuambukiza hivi sasa kila mtu anakunywa pombe hiyo kwa kutumia chombo chake.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo

1 comment:

Unknown said...

mi nimependa sana maamuzi yako Mponzi ya kutaka kuweka kumbukumbu za kabila la wasafwa. kiukweli sisi hatuendelei kwasababu tumeacha asili yetu na kukumbatia asili za wengine ambazo nazo hatuzijui vizuri.

Mfano China na Korea zote mbili hawakukubali kuingiliwa na tamaduni za kizungu na ndio maana wameendelea kwani walisimamia utamaduni wao.

"Mjasiri haachi asili"

Viva Mponzi Viva!

Mbwanyizanye bernard yobele njelwa