Akina mama wanamsindikiza kwa kumzomea mtuhumiwa huyo
Mkazi wa Mtaa wa Mbete,Kata
ya Isanga Jijini Mbeya Bwana Yussuf Hamad(39),anatuhumiwa kumpa mimba binti
yake wa kumzaa(15) jina lake limehifadhiwa.
Hayo yamethibitishwa na Mama mzazi
wa binti huyo Bi, Regina Simon(35) baada ya kupata taarifa Mei 11 mwaka huu
kuwa binti yake ana ujauzito wa miezi minne,na kuamua kutoa taarifa kwa
Balozi wa mtaa huo Bwana Steven Ovaova ambaye naye alitoa taarifa kwa
Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Angelo Sanga.
Viongozi hao wa mtaa
walimuita mtuhumiwa na ili kupata ukweli wa tukio hilo,lakini mtuhumiwa
alikanusha ingawa binti yake alithibitisha kutendewa ukatili huo na kwamba
alikuwa akitishiwa kwa mapanga kila alipokuwa akifanya naye tendo la ndoa.
Baada ya uongozi kupata maelezo
kutoka kwa binti huyo na mzazi kukataa waliamua kuipeleka kesi hiyo
Polisi,ambapo walitoa PF3 iliyomwezesha binti huyo kupelekwa kwa
No comments:
Post a Comment