Hawa Mathias,Mbeya.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imejipanga na kuweka mikakati kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na hali ya usafi wa mazingira nchini na kuhakikisha jamii inatumia vyoo safi na salama na kuondokana na adha ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko hususan kipindupindu.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi msaidizi,afisa afya mkuu Tanzania wa wizara ya afya na ustawi wa jamii Elias Chinamo katika maadhimisho ya siku ya choo duniani yaliyofanyika wilayani rungwe Mkoani Mbeya.
Alisema kuwa ili kufikia malengo ya mileniam ya utunzaji wa usafi wa mazingira jamii inatakiwa kuwa na mwamko wa kujikita katika kutunza hali ya mazingira na kujenga vyoo bora ili kuondokana na adha ya kusambaa kwa vinyesi vinavyochangia kusababisha magonjwa ya milipuko na kuhara.
Aidha alisema kuwa katika kufanikisha maadhimisho hayo na tumeweka mikakati ya kufikisha ujumbe kwa wananchi kwa kutoa elimu ya usafi wazingira na matumizi ya vyoo bora kupitia vipeperushi ,na vyombo vya habari.
"Pia tumeandaa mashindano ya usafi wa mazingira katika shule za msingi na sekondari ,kata na kaya,na taasisi mbalimbali binafsi na serikalini"Alisema.
Chinamo alifafanua kuwa hali ya usasi wa mazingira ya vyoo bora bado ni changamoto kubwa nchini na kwamba jitihada za pekee za hitajika kwani takwimu zinaonyesha asilimia 12 pekee ya kaya nchini ndizo zenye vyoo bora na salama kwa afya za watumiaji.
No comments:
Post a Comment