PETRO S/O SANGA,MIAKA
25,MKULIMA,MKINGA MKAZI WA CHAPAKAZI – MBALIZI ALIFARIKI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
MAREHEMU ALICHOMWA KISU SHINGONI NA
MDOMONI NA KIKUNDI CHA WATU WANAOSADIKIWA KUWA ASKARI WA JESHI LA
WANANCHI WA TANZANIA [JWTZ] KIKOSI CHA 44KJ MBALIZI TAREHE 18.11.2012 MAJIRA YA
SAA 21:00HRS AKIWA KATIKA GROCERY IITWAYO VAVENE MWE ILIYOPO
MBALIZI.
MARA BAADA YA WATU HAO KUVAMIA
BAR IITWAYO POWER NIGHT CLUB AMBAMO AWALI ALIKUWEPO PIA MAREHEMU.
WAHALIFU HAO WALIANZA KUWASHAMBULIA
WANANCHI KWA KUWAPIGA WAKITUMIA NGUMI, MATEKE, MIKANDA, MARUNGU, SIME NA
MAPANGA.
MAREHEMU ALIJARIBU KUOKOA UHAI
WAKE KWA KUKIMBIA TOKA ENEO HILO HADI KATIKA GROSARY HIYO LAKINI
WATU HAO WALIMKIMBIZA HADI ENEO HILO NA KUMJERUHI VIBAYA KWA KUMCHOMA KISU.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI KULIPIZA
KISASI KUFUATIA ASKARI GODFREY S/O MATETE,MIAKA 30,MJITA, WA KIKOSI CHA 44KJ
MBALIZI KUPIGWA NA WALINZI WA KILABU CHA POMBE ZA KIENYEJI KIITWACHO DDC
KILICHOPO MBALIZI WALIOKUWA LINDONI TAREHE 17.11.2012 MAJIRA YA SAA
01:30HRS.
BAADA YA KUSHAMBULIWA ASKARI
HUYO ALIFUNGUA KESI KITUO CHA POLISI MBALIZI USIKU HUO KOSA – KUJERUHI NA
ALIPATIWA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA KUPATA MATIBABU
HOSPITALINI .
WALINZI WANNE WALIKAMATWA
KUHUSIANA NA TUKIO HILO KWA MAHOJIANO AMBAO NI 1. FRENK S/O
MTASIMWA, MIAKA 25, MHEHE 2. MURE S/O JULIAS, MIAKA 26, MMALILA 3. OMARI S/O
CHARLES, MIAKA 28, MMALILA WOTE WAKAZI WA DDC MBALIZI NA 4. LEGNARD S/O
MWAMPETE, MIAKA 30, KYUSA MKAZI WA IZUMBWE. UPELELEZI WA KESI HIYO BADO
UNAENDELEA.
AIDHA TAREHE 18.11.2012 WATU
WENGINE SITA WALIJERUHIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI
YAO NA WANAODAIWA KUWA ASKARI WA JWTZ NA KUPATIWA HATI YA MATIBABU [PF3]
KWA MATIBABU. KATI YAO WATATU WALILAZWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA IFISI KWA
MATIBABU ZAIDI.
MAJERUHI WENGINE WATATU WALIPATIWA
MATIBABU NA KURUHUSIWA. AIDHA KUFUATIA VURUGU HIZO BAADHI YA MALI ZA WATU ZILIHARIBIWA
AMBAZO NI PAMOJA NA 1. GARI T.106 AWB AINA YA TOYOTA VISTA MALI YA PAULO S/O
MAXIMILIAN ILIVUNJWA KIOO CHA MBELE 2. GARI T.884 AUU TOYOTA CRESTA MALI YA
ALILE S/O GODFREY LILIVUNJWA SIDE MIRROR UPANDE WA KULIA.
MWILI WA MAREHEMU ULIFANYIWA UCHUNGUZI
NA DAKTARI WA SERIKALI NA KISHA KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA AJILI YA TARATIBU ZA
MAZISHI.
HATA HIVYO UPELELEZI WA KESI HII BADO
UNAENDELEA AMBAPO JUMLA YA ASKARI KUMI [10] WA KIKOSI CHA 44KJ MBALIZI
WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIO HILO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA TABIA
YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA PINDI WANAPOTENDEWA ISIVYO HALALI NI VIZURI
KUTOA MALALAMIKO YAO KATIKA MAMLAKA HUSIKA .
VILEVILE ANATOA RAI KWA
JAMII KUJENGA TABIA YA KUTII SHERIA BILA SHURUTI.
KAMANDA DIWANI ANATOA POLE KWA
NDUGU JAMAA NA MARAFIKI WA MAREHEMU PETRO S/O SANGA KWA MSIBA MZITO
ULIOWAKUTA NA KUWATAKA KUWA NA MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU
WALICHONACHO KWANI SERIKALI, JESHI LA POLISI LINAFANYA JITIHADA ZA DHATI
KUHAKIKISHA HAKI INATENDEKA KWA MUJIBU WA SHERIA.
TAARIFA ZAIDI YA MATUKIO HAYA
ITAENDELEA KUTOLEWA. KWA SASA HALI YA MJI WA MBALIZI NI SALAMA, WANANCHI
WANAENDELEA NA SHUGHULI ZAO ZA KAWAIDA KUTAFUTA MAENDELEO.
Signed By,
[DIWANI
ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment