Hawa Mathias,Mbeya.
Jeshi la polisi Mkoani Mbeya linawashikiliwa watu wawili akiwemo mwanamke wakazi wa kijiji cha Madibila na Mkunywa Wilayani mbarali kwa tuhuma za kupatika na silaha pamoja na nyara za serikali kinyume cha sheria.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Athuman Diwani alisema kuwa watuhumiwa hao walikamtwa kwa nyakati tofauti na askari wa wanayamapori (TANAPA) na akari wa jeshi la polisi walipokuwa katika doria za kusaka waharifu
Alisema kuwa katika tukio la kwanza Christian Mhangole (40) mkulima alikamatwa na polisi akiwa na siraha aina ya SMG yenye namba 88560 ikiwa na risasi 50 ambazo zilikuwa zimehifadhiwa katika mfuko maarufu kama( sulphet ).
Diwani alisema kuwa mara baada ya uchunguzi zaidi mtuhumiwa huyo alibainika kuwa na nyara za serikali ikiwa ni pamoja na nyama ya nyati kilo 15 ,nyama ya tembo kili 17 ambazo zilikuwa zimefichwa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kwamba siraha aliyokamatwa nayo imekuwa ikimilikiwa kinyume cha sheria.
Aidha kamanda Diwani alisema mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kujihusisha na biashara ya uwindaji haramu wa wanyama pori na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi kukamiliki kujibu tuhuma zinazomkabili.
Katika tukio la pili mwanamke kijiji cha Mkunywa wilayani mbarali Emaliana Ndemo (30) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kupatikana na siraha aina ya Reffle yenye namba B 58221 ikiwa imefichwa chumbani ndani ya nyumba yake .
Diwani alifafanua kuwa kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kulitokana na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na jeshi la polisi na kwamba ilikuwa ikitumiwa na mume wa mtuhumiwa aliyejulikana kwa jina za moses mlingamolo (30) ambaye alifanikiwa kukimbia na polisi wanaendelea na msako ili aweze kufikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria.
Aidha kamanda wa polisi ametoa wito kwa wananchi kuwafichua watu wanaomiliki siraha kinyume cha sheria kwani wanachangia uvunjifu wa amani kwa wananchi wasiokuwa na hatia na kwamba watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.
No comments:
Post a Comment