KITUO CHA ORXY
VIJANA WA BODA BODA WAKIWA WAMEVAMIA KITUO CHA ORXY KUTAKA KUJUA KAMA KWELI KUNA MAFUTA AMA LAH.
HAPA KILA MTU ANATAKA KUSHUHUDIA KAMA MAFUTA YAPO AMA LAH
MENEJA WA KITUO HICHO ALIYE VAA SHATI JEUPE AKIJARIBU KUWATULIZA WATEJA AMBAO WANA JAZBA KUBWA YA KUTAKA KUJUA KAMA KUNA MAFUTA AU LAH , NA KUWAMBIA KUWA WANGOJE KWANZA ACHUKUE VIFAA ILI AWAONESHE KUWE KWELI HAKUNA MAFUTA.
MKUU WA POLISI WILAYA YA MBEYA NAE ALIKUWEPO ENEO LA TUKIO,KUWATULIZA VIJANA HAO NA KUWAHAKIKISHIA KUWA WATAONESHWA KUWA KWELI HAKUNA MAFUTA KATIKA ENEO HILO.
HAPA KATI KATI WANAPO TAZAMA NDIPO KWENYE TANK LA MAFUTA , VIJANA WANANGOJA KUSHUHUDIA.
KAZI INAANZA SASA YA KUTAZAMA KUWA MAFUTA YAPO AMA HAYAPO, AMBAPO CHUMA MAALUM KINAINGIZWA KATIKA MATANK HAYO SASA
SASA VIJANA WANAHAKIKISHIWA KUWA MAFUTA AINA YA PETROL HAKUNA KATIKA KITUO HICHO CHA ORXY
HII NI FOLENI AMBAYO IMEPIGWA WATU KWENDA KUNUNUA NAFUTA
HII NDIO INAITWA KUFA KUFAANA WAKATI WENGINE WAMEGOMA KUUZA MAFUTA VIJANA PEMBENI WAMEJIPATIA AJILA YA KUUZA MAFUTA AMBAPO KWA LITA MOJA NI FEDHA ZA KITANZANIA 20,000
HAPA MTEJA ANAONDOKA NA LITA ZAKE 5 KWA TSH 20,000
KITUO CHA TOTAL MBEYA MUDA MCHACHE ULIOPITA
HALI HAPA PIA NI TETE SANA KAMA INAVYO ONEKANA MADEREVA WAKIWA NA BODABODA ZAO KUTAKA MAFUTA
KITUO CHA BP MBEYA MJINI
HII NDIO HALI HALISI YA KITUO CHA BP MBEYA MAGARI YOTE BINAFSI NA SERIKALI YAMEPANGA FOLENI KUNUNUA MAFUTA
WATU WAKIWA WAMECHOKA KUNGOJEA MAFUTA
MAGARI YA FIRE(ZIMA MOTO NAYO YAPO )
MZEE MANJI AKIWA ANATAZAMA SHUGHURI NZIMA YA UUZAJI WA MAFUTA
HUU NI MTAA WA WEST STREET AMBAPO MAGARI PAMOJA NA BODA WAMEPANGA FOLENI KUNUNUA MAFUTA
KITUO CHA TOTAL JIJINI MBEYA
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG
1 comment:
Maisha Bora Kwa Kila Mtandhania
Post a Comment