*Binti huyo yadaiwa ni Mke wake.
*Mchungaji huyo atoa sh. 20,000/=
ili binti aitoe mimba hiyo.
*Askofu afuatilia sakata hilo.
Mchungaji wa Kanisa la Reedemed
Gospel Church John Mgalah(38) lililopo Kijiji cha Namlonga, Kata ya Ruanda,
Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya, anadaiwa kumpa mimba muumini wake Mariam
Mwakabata(18), Mkazi wa Kijiji cha Idibila Wilayani humo.
Tukio hili ni kufuatia muumini huyo
kudai alipigiwa simu na mchungaji huyo mnamo Selida Mtafya mwenye watoto sita
akiwa amekwenda wilaya ya Mbeya katika Hospitali ya Ifisi kupatiwa matibabu.
Mariam amedai kuwa aliwasili
kijijini hapo akitokea Mji mdogo wa Tunduma, alipokuwa amekwenda kuwasalimu
kaka zake majira ya saa 11 wakati mchungaji akishiriki harusi ya Bwana Mika
Msolina iliyokuwa ikifungwa kanisani hilo.
Aidha binti huyo amedai kuwa
mchungaji alimtaka kutangulia nyumbani kwake naye kuitikia wito wa mchungaji,
ambapo aliwasili saa 3:00 usiku na mchungaji kuwasili majira ya saa 4:00 usiku
na kumtaka binti aende nyumba ya nje na kisha kukubali na mara
baada ya mchungaji kufika alianza kumtomasasehemu mbalimbali, hali ambayo
ilimfanya binti huyo kupiga kelele na mchungaji kutoka nje.
Mchungaji alirejea mara ya pili
ndani ndipo alipofanikiwa kumbaka na kumsababishia ujauzito sasa ni miezi
mitatu.
Baada ya kupitia mwezi mmoja kupita
Binti huyo alimpigia simu mchungaji na kumueleza hali halisi ambapo
alimtaka binti huyo kuitoa mimba na kumpa shilingi 20,000, lakini Mariam
alipokea pesa hizo lakini hakwenda kuitoa mimba hiyo.
Binti huyo alianza kuutaarifa
uongozi wa kanisa kufuatia mimba hiyo hiyo ndopo mchungaji alianza na yeye
kukamilisha mchungaji alianza naye kukamilisha kumpa ujauzito huo.
Kwa upande wake Mchungaji
alikanusha kuhusika na tendo hilo na kwamba binti uyo ana nia ya kumchafua tu
ingawa binti huyo kulala kwake siku hiyo ya harusi na kudai alikuwa na ugomvi
wa na familia yake.
Hata hivyo Askofu wa Kanisa hilo,
Tawi la Mlowo wilayani humo Anyimike Mwaitumile amekiri kupokea shauri hilo na
kwamba wanafanya uchunguzi na pindi atakapobainika watamchukulia hatua za
kinidhamu kwa mtumishi huyo na kwamba wachungaji wa kanisa hilo wanatakiwa
kujiepusha na mabinti kwani wanaweza kuwatondosha katika imani.
Wakati huo huo Serikali ya
Kitongoji kupitia Bwana Asaulile Mwakimwili amesema kuwa suala hilo lipo
kwenye Ofisi yake na wameweza kukutana na pande zote mbili na Mchungaji
kukanusha lakini suala hilo likiwa limefikishwa katika Ofisi ya serikali ya
kijiji chini ya Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Asavule Mwakimwile na Afisa Mtendaji
wa kijiji Bwana Beck T Siwale na kudai kuwa wanachosubiri barua ili sheria
iweze kuchukua mkondo wake.
Na Ezekiel Kamanga, Mbozi
No comments:
Post a Comment