Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiwa na wadau wa Czech BEZ MAMY |
Michoro ya picha za tingatinga inayotumika kukusanya michango hiyo |
Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia akiendesha moja ya semina za kuchangia mfuko huo
Shirika lisilo la
kiserikali la Jamhuri ya Czech BEZ MAMY limeanza kampeni ya kukusanya pesa Ulaya
kwa ajili ya Kusaidia watoto yatima nchini Tanzania hasa mkoani Mbeya
Bez Mamy kwa
kushirikiana na shirika la Kitanzania la jiji Mbeya Without Mother Organization
kwa pamoja wamedhamiria kuinua elimu mkoani Mbeya kwa kusaidia ukarabati na
utoaji wa misaada kwa shule za msingi jijini Mbeya, Ujenzi wa vituo vya watoto
yatima, kuwalipia ada watoto yatima na kuboresha huduma za Afya jijini na
wilaya mbalimbali za mkoa wa Mbeya
Akiongea na blog hii
Mratibu wa miradi na Mwakilishi wa Bez Mamy Africa Bw Chris Zacharia alisema,
wanatumia njia mbalimbali kukusanya pesa
hizo ambazo zitatumika katika ujenzi wa Bweni la wasichana katika kituo
cha watoto yatima Mahango,Mswiswi pamoja na ujenzi wa Sekondari ya Ufundi
katika Kijiji hicho cha Mahango
Njia zinazotumika
kukusanya pesa hizo ni uuzaji wa michoro ya Tinga Tinga katika sehemu
Mbalimbali nchini Slovakia na Jamhuri ya Czech na pia kupitia mtandao www.tingatingashop.cz
Njia nyingine ni
utoaji wa Mihadhari katika vyuo vikuu, shule za sekondari za ufundi, Makanisani
na kwa watu binafsi katika nchi hizo
Akizungumzia misaada
na miradi hii bwa Chris Zacharia alisema,Ikiwa watu wa Ulaya wanajitoa kusaidia
watoto wa afrika itawatia moyo zaidi kusaidia ikiwa watasikia watanzania
wengine wenye uwezo pamoja na serikali wanajitoa kusaidia kundeleza miradi hii
ambayo ina msaada mkubwa kwa uchumi na maeneleo ya nchi yetu
|
No comments:
Post a Comment