Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu
Maelfu ya watu wakiongezeka kuja katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi Muda huu
Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali
Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu
Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliye jishika, akiwa na uchungu muda huu
Ibada ikiwa inakaribia kuanza
Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa
Waandishi wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .
Endelea kufuatilia Moja kwa moja hapa
PICHA ZOTE NA MBEYA YETU BLOG
2 comments:
poleni sana watanzania wenzangu kwa msiba uliotukuta.
kuna umuhimu sana kwa viongozi wetu wa vyama vya siasa, serikari pamoja wakuu wote wa idala kupelekwa semina na kuhelimishwa kuwa uwepo wao unategemea ss
Hakuna Msiba unaoniuma kama Huu wa Daudi Mwangosi. Kulipuliwa kwa bomu tumboni tena kwa kukusudia na polisi ambaye alitakiwa awe mtu wa kumlinda.
Nachelea kusema tukio hili siyo bahati. Natukio la makusudi, na nahisi ni tukio lililopangwa maana kuna dalili kuwa uhusuano kati ya polisi na waandishi wa habari Iringa siyo mzuri. Na vile nahisi mwangosi alikuwa mwiba sana kwa hawa jamaa wasiopenda kuwatendea haki watanzania yani polisi na mafisadi wao.
Hakika wamemua mwandishi wetu lakini wajue hapa duniani wote tunapita. Na dhuluma haiwezi kushinda haki. Tuna amini malipo ya uovu wa huu yatalipwa hapahapa duniani ai ahela.
Naomba Mungu amlaze mahali pema mpendwa wetu apumzike kwa amani.
Post a Comment