Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Wednesday, August 15, 2012

CWT YAONYA WALIMU WANAOJIANDAA KUVURUGA SENSA


CHAMA cha walimu Tanzania (CWT) kimesema kuwa hakipo tayari kuwatetea walimu walioengeliwa majina yao katika zoezi la kusimamia Sensa mwaka huu na kujiandaa kuvuruga zoezi hilo.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Kaimu Katibu wa CWT Taifa Ezekiah Oluoch alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Tunduma baada ya kujionea uharibifu wa ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mji mdogo wa Tunduma iliyovunjwa siku ya mgomo wa walimu.

Oluoch alisema kuwa licha ya CWT kuwa na nyaraka za kuenguliwa kwa baadhi ya walimu katika zoezi hilo, amewataka walimu kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo na kwamba mwalimu ambaye atabainika kuhujumu zoezi hilo Serikali imshitaki kama mhalifu mwingine.

Akizungumzia suala la kulipa fidia za uhalibifu wa jengo na wizi wa mali za ofisi ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma uliotokana baada ya wanafunzi kufika eneo hilo na kudai haki ya kufundishwa siku ya mgomo wa walimu Juni 30, mwaka huu, alisema CWT haipo tayari kulipa kwasababu hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa walimu ndiyo waliohusika na uhalifu huo.

Alisema uchunguzi wa Serikali ukibaini kuwa kuna walimu waliohusika kuwashawishi wanafunzi kuandamana mpaka katika ofisi hizo, basi walimu hao wawajibike wao kama wao na endapo kuna walimu walishiriki moja kwa moja katika kuvunja ofisi na kuiba mali za ofizi hiyo CWT watalipa na si vinginevyo.

‘’Ninachoweza kusema kwa niaba ya CWT ni kutoa pole kwa uongozi wa Mamlaka kwa kuvunjiwa ofisi na kuibiwa samani na kikundi cha wahuni na tunalaani tukio lililotokea, lakini kwasababu CWT na ofizi Mamlaka ni majirani mwema tutakapopata tathimini ya uhalibifu huo tutatoa kifuta machozi lakini siyo fidia ya ujumla other wise Serikali itupeleke mahakamani’’ alisema Oluoch.

Sanjari na hayo alisema kuwa Serikali haikitendei haki chama cha walimu kwa kuwahusisha viongozi wake kuwa wanafadhiliwa na Chadema kwa ajili ya kuvuruga amani ya nchi na kwamba ikithibitisha suala hilo yeye atakuwa kiongozi wa kwanza kujiuzulu wadhifa wake na kurudi kufundisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mji wa Tunduma Aidan Mwasiga alisema kuwa uhalibifu uliotokea siku ya mgomo wa walimu nchini CWT hawawezi kukwepa lawama kuwa chanzo cha uhalibifu wa ofisi yake na wizi na kwamba wala suala hilo halihusiani na Siasa.

Alizitaja baadhi ya athari kubwa zilizopatikana bada ya ofisi yake kuvunjwa na kuibwa baadhi ya vitu kuwa ni pamoja na mji huo kukosa ushuru kutokana na nyaraka zote za kiserikali kuibwa vikiwemo vitabu vya kukusanyia mapato ya mji huo.

Habari kwa hisani ya Kalulunga

1 comment:

Anonymous said...

Tumechoka kila siku kutoa tuhuma bila kuwataja wahusika, si muwataje?