Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Binti wa kazi za ndani aliyefahamika kwa jina moja la Zefa(8),mkazi wa Mtaa wa Block Q - Makunguru,Kata ya Ruanda Jijini Mbeya amefariki dunia akiwa chumbani kwa usiku wa manane Mei 30 mwaka huu.
Binti huyo aliyefika siku nne zilizopita akitokea Kijiji cha Msangano, Wilaya ya Mbozi alikuwa akifanya kazi kwa Bwana Veramundi Mtally mkazi wa mtaa huo.
Tukio hilo limetokea Mei 30 mwaka huu mara baada ya kumaliza kupika,binti huyo aliongeza mkaa na kisha kulala na mtoto huyo wa mwajiri wake aitwaye Goodluck Veramundi(7),ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Kambalage jijini hapa.
Mnamo majira ya asubuhi saa 12:00 jioni Bwana Mtally aliingia chumba cha binti huyo kwania ya kumwamsha ili amuandae mtoto kwa ajili ya shule ndipo aligonga mlango bila kupata majibu na kisha kugonga dirisha pia hakufanikiwa ndipo alipoamua kuuvunja mlango na kumkuta binti huyo akiwa hajitambui pamoja na mtoto aliyekuwa naye chumbani.
Bwana Mtally aliomba msaada kwa balozi wa mtaa huo kusaidia kutoa nje mwili wa marehemu Zefa pamoja na mtoto Goodluck na kuwapeleka katika Hospitali ya Rufaa jijini hapa na walipofika Daktari wa zamu alibainisha kuwa binti huyo amefariki.
Aidha mtoto huyo amenusurika kifo kutokana na kujifunika blanketi gubigubi hivyo hewa yenye moshi haikuweza kumpata,licha ya kukutwa akiwa mchovu na hajitambui.
Hata hivyo Bwana Mtally alitoa taarifa Kiyuo cha polisi kati na kupewa PF3 na hivyo kuruhusiwa kutibiwa na kulazwa mwanawe katika hospitali ya Rufaa.
Mwili wa marehemu Zefa umehifadhiwa Hospitalini hapo,ukisuburi ndugu zake kutoka Msangano kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Wakati huohuo katika msimu huu wa baridi kali mkoani hapa wamekuwa wakitumia nishati ya mkaa hali inayohatarisha maisha ya wakazi wengi ambao hutumia mkaa kupikia na kuota ili kujisitili na baridi.
Jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi wa tukio hilo la kusikitisha na kukuta mkaa ukiwa unawaka huku maji yakichemka,madirisha yakitoa mvuke kutokana na joto kali lililokuwepo katika chumba hicho.
1 comment:
Maskini,hivi kwa nini waajiri wasiwe wanawaelimisha wasichana wao wa ndani hasa wageni wanaotoka mbali (nje ya mikoa ambayo inabaridi)...hayo matukio yametokea mengi sana jiji mbeya nakumbuka kipindi nipo mdogo jijini Mbeya.
Poleni sana wafiwa.
Post a Comment