Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Hatimaye Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekamilisha taratibu zote za kukipandisha hadhi Kituo cha afya cha Igawilo, kilichopo jijini hapa kuwa Hospitali.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Idd ameiambia Bomba Fm kuwa tayari Halmashauri ya Jiji imepokea cheti cha kupandishwa hadhi kwa kituo hicho cha afya na kuwa ifikapo Julai Mosi mwaka huu kituo hicho kitatambuliwa rasmi kuwa ni hospitali.
Amesema hadi sasa kituo hicho cha afya kinatoa huduma zote kama hospitali isipokuwa kinachosubiriwa ili kuiita hospitali ni muda tu ufike kwa mujibu wa sheria.
Aidha, Idd ameiambia bomba fm kuwa hospitali hiyo inatarajiwa kutoa huduma kwa wakazi wote wa bonde la Uyole, Mbeya Vijijini, kata a jirani na wananchi wote kwa ujumla kwa kuwa huduma za afya huwa hazina mipaka ya kiutawala.
No comments:
Post a Comment