Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 8, 2012

ANAHITAJI KUSAIDIWA: MAMA MWENYE MATATIZO YA AKILI AZALISHWA WATOTO SITA NA WATU TOFAUTI ASIO WAJUA.

 Mama Rebeka Mbwiga mkazi wa Uyole akiwa na mtoto wake wa sita Japhet 

 Mtoto Japhet akiwa Mwenye afya Njema akifurahi kuona Camera ya Mbeya yetu mapema leo 

Mama Japhet akiwa anaondoka mara baada ya kukumbana na Camera yetu moja kwa moja Jijini Mbeya

********
Mama Rebecca Mbwiga ni Mwanamke ambaye ana matatizo ya akili, na ambaye alikuwa na watoto sita na sasa wamebakia wa tano kutokana na mmoja kati ya hao Kufariki Dunia.
Mama huyu anahitaji msaada wako wa Hali na mali kutokana na kwamba hawa wote walio mzalisha ni watu ambao hawajulikaniki kabisa. wamekuwa wakimpa Mimba na kuondoka.
Taarifa kamili zinasema kwamba Binadamu hao wanyama humwendea mwanamke huyo sehemu anayo lala usiku na ku Mbaka, Jambo lililo mpelekea kuwa na watoto wote hao sita.
Wengi wa wakazi wa jiji la Mbeya wanamfahamu mwanamke huyu Rebecca, kwa kuwa huwa anapita ofisi mbali mbali mjini kuomba msaada.
Hata hivyo Rebecca amesema kuwa watoto wake wanne kwa sasa wanajitegemea wenyewe na maisha yao kwa kazi hiyo hiyo ya kuomba.

Mbeya yetu inaendelea kufuatilia mpaka makazi yake yaliyopo, na pia Tunawaomba kwa wale wote wa maofisini pamoja na wadau wote mnao Mfahamu Mama huyu mpate kumpa msaada maana ana viumbe ambao wamepatikana si  kwa yeye kupenda bali ni kutoka kwa wale ambao wanatamani Ngono.
Pia tumnusuru mama huyu na Gonjwa hatari la UKIMWI pamoja na  Magonjwa ya zinaa


1 comment:

Bufa said...

dah! inasikitisha kwakweli.