Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, June 8, 2012

Kamera ya Mbeya Yetu yakutana ana kwa ana na Muuza miwa anaye tumia piki piki Mtaani, na kufanya nae Mahojiano mafupi

 Muuza Miwa maarufu akiwa anakatiza West Street jijini Mbeya  mapema leo 
 Muuza Miwa maarufu akiwa anapanga miwa yake leo 
 Miwa ikiwa tayali kwa ajili ya kufanyiwa mauzo leo 
 Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog  Joseph mwaisango aliye vaa shati Jeupe akifanya mahojiano na Muuza miwa huyo 
 Muda mchache baada ya kufanya mazungumzo Wadau walianza nunua Miwa eneo hilo 
 Mwandishi wa Mbeya yetu Joseph Mwaisango Kulia akiwa na muuza miwa Pamoja na mdau mwengine wakipata miwa kutoka kwa mdau
Baada ya Mazungumzo na Mbeya yetu mdau aliondoka zake
***********************
Mbeya yetu leo katika Kodoa kodoa na Kamera yetu ilipaya bahati kuonana Live na Bwana Mecky ambaye ni muuza Miwa maarufu jijini Mbeya. Ambapo alipo hojiwa alisema "Kwa kweli miwa hii naifuata kule Usangu ambapo nanunulia kwa bei ya kule kule, Lakini miwa hii pia huwa naisambaza hapa jijini pamoja na vitongoji vyake". Aliongeza na kusema kuwa "Watu wengi wanaidharau sana  biashara hii ambayo inaniingizia kipato kikubwa" Mwisho akamalizia kuwa "Nawashauri vijana wenzangu msilalamike kuwa hakuna ajira wakati kazi zipo nyingi" 
Baada ya hapo aliondoka zake

No comments: