Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Ajali za barabarani zimeendelea kuchukua sura Mkoani Mbeya,baada ya kutokea ajali iliyoua watu 13 wiki moja iliyopita,baada ya gari aina ya Coaster na Lori iliyotokea eneo la Iwalanje,Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Juni 14 mwaka huu majira ya saa 12:30 asubuhi katika eneo la Iwambi(Stelah Farm) gari aina ya Toyota Hiace yenye nambari T 247 BUF liligongana na Lori kwa nyuma lenye nambari T 786 BBH linalimolikiwa na Kampuni ya Malumalu ya Marmo Grabito Mines ya jijini Mbeya,kisha Hiace hiyo kugonga Lori jingine lenye nambari T 699 BXU lililokuwa na tela nambari T 233 AFC.
Hiace hiyo iliyokuwa kwenye mwendokasi imesababisha abiria zaidi ya 18 wakiwemo wanafunzi kadhaa wa shule za sekondari waliokuwa wakienda mashuleni mwao kujeruhiwa,waliokuwa wakitokea Mwanjelwa kuelekea Mbalizi nje kidogo ya jiji.
Aidha,gari hilo la abiria limeharibika vibaya na baadhi ya abiria kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa na ya Mkoa zilizopo jijini Mbeya.
Miongoni mwa abiria waliokuwa katika hali mbaya ni wanafunzi wawili ambao shule wanayosoma na makazi yao kwa sasa hayajafahamika kutokana na kujeruhiwa vibaya hali iliyowasababishia kuvuja damu nyingi.
Hata hivyo abiria waliokuwemo katika Hiace hiyo waliathiriwa na pombe ya kienyeji maarufu kwa jina la Kimpumu iliyokuwemo kwenye gari hiyo,baada ya ndoo zilizokuwa zimetumika kubeba pombe hiyo kupasuka na kufanya gari nzima kutapakaa,ambapo madaktari na wauguzi walikuwa katika wakati mgumu kukabiliana na harufu ya pome hiyo.
No comments:
Post a Comment