Habari na Ezekiel Kamanga.
Wanawake wawili wajitokeza kugombea nafasi ya Urais na Makamu Rais.
Kampeni za uchaguzi wa
kumpata Rais wa Chuo kikuu cha Teku, zimezinduliwa rasmi jana katika
ukumbi wa Mwasakafyuka huku wagombea wakinadi sera zao.
Kampeni hizo zilizinduliwa
na Dakta Mozes D, na kusimamiwa na mkufunzi wa chuo Bwana Alawi
Mikidadi ambapo Mkurugenzi wa uchaguzi Bi Nyemba Joyce aliweka hadharani
wagombea watakao wania viti vya urais na makamu rais.
Majina hayo upande wa rais
ni Bi Somi Irene, Bwana George Godbless na Joshua Jason na upande wa
Makamu ni Bi Wilson Gwantwa, Bwana Yohanna Yesse na Deus Petro.
Mwenyekiti wa tume ya
uchaguzi Bwana Kavenga Emmanuel amesema kwamba mchakato wa uchaguzi
ulianza Mei 9 mwaka ahuu kwa kujaza fomu ambapo wanachuo 70 walijitokeza
kuomba nafasi mbalimbali.
Aidha Mei
19 na 20 wagombea walifanyiwa wagombea usaili na kwamba majina
yaliyotajwa hapo juu ndio yaliyopitishwa na tume hiyo na kwamba kampeni
zimeanza rasmi jana ambazo zitaendelea mpaka Mei 28 asubuhi na uchaguzi
utafanyika Mei 29 mwaka huu na matokeo yatatangazwa mei 30 mwaka huu na
viongozi wote Rais na baraza la mawaziri kuapishwa Juni mosi mwaka huu.
Mwenyekiti huyo Bwana
Kavenga amewataka viongozi hao kufanya kampeni za amani bila matusi
kwani kampeni kwa kufanya hivyo haitawasaidia kupata kura, bali
itawashushua heshima zao.
Kwa upande wake Rais
anayemaliza muda wake Bwana Ambukege Imani ameishukuru tume ya uchaguzi
kwa mchakato mzima na anafurahi kumaliza muda wake chuo kikiwa na amani
na kuwataka watakaopata nafasi za kuongoza wazingatie sheria, demokrasia
na upendo ili kuleta mshikamano katika chuo, ili wanaoongozwa wajisikie
kuwa na amani kuwepo chuoni hapo badala ya kutatua migogoro isiyokuwa
na maana.
Baadhi ya wabunge walipita bila kupingwa, kutokana na baadhi ya maeneo waliyokuwa wakiyagombea kutokuwa na wapinzani.
Hata
hivyo kujitokeza kwa wanawake kumeleta msisimko wa uchaguzi huo huku
wanawake wakitoa majigambo kuwa wanawake wanaweza hata pasipo kuwezeshwa
na kwamba chuo hicho hakijawahi kupata viongozi wa juu ambao ni
wanawake na kwamba imefika zamu yao kuongoza.
No comments:
Post a Comment