Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, April 20, 2012

KAMERA YETU LEO IMEMULIKA MOJA KWA MOJA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA , WAONA WAGONJWA WALALAMIKA KUWA HAWANA HUDUMA YA CHOO WALA MAHALI PA KUPUMZIKA PINDI WANAPO NGOJA KUWATAZAMA WAGONJWA

 Hili ni Lango kuu la kuingilia Hospitali ya Rufaa, ambapo wananchi wamekaa pembeni tuu hawana mahali maalum pa kupumzikia 
 Baadhi ya wananchi wakiwa pembeni kabisa bara bara ya kuelekea kituo cha polisi wakingojea kuwaona Ndugu zao
 Kila mtu anaonekana anatafuta eneo la kujisitili wakati wanangoja kutazama wagonjwa 
Hapa ni eneo la kanisa la Katoriki lililopo jirani na hospitali ya Rufaa, Eneo hili hutumika kwa wakazi hao kujisitili pale mvua inapo nyesha

*****
Wakazi wa Jiji la Mbeya na wanao toka maeneo ya jirani wamelalamika vikali kuwa hospitali ya Rufaa haiwajali kwa kuto wawekea huduma muhimu kama ya Choo na sehemu ya kupumzika pale wanapo ngoja kuwaona wagonjwa wao.
Wakizungumza na na mtandao huu moja kwa moja wamedai kwamba wana wakati mgumu sana hasa pale mvua zinapo anza kunyesha jambo linalo sababisha wao kulowana na hata kuumwa, Pia wamedai kwamba hata wakiingia humo ndani vyoo ni vichafu ambapo pia vinasababisha kuhatarisha afya zao.
Mwisho wameiomba hospitali hiyo  kuwasaidia kupata hudumahiyo mapama iwezekanavyo, ili kuepusha usumbufu huo.

No comments: