Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Sunday, March 18, 2012

Live sasa hivi: Mabloga wakongwe Nchini ana kwa ana na Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu Blog Muda huu.

Kutoka kushoto ni Ahmad Michuzi A.k.a Michuzi Jr ambaye anamiliki Libeneke la Jiachie Anae fuatia ni mzee wa Mji kasoro Bahari Mroki Mroki ambae libeneke lake ni Father Kidevu wa tatu kutoka Kushoto ni Joseph Mwaisango Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu na Mwisho ni John Bukuku anae miliki Libeneke la Full Shangwe 
Gari la wanalibeneke Hao Likiwa linaondoka kutoka Mbeya kuelekea Iringa Muda huu, Mbeya yetu Blog pamoja na wadau wote Tunawatakia Safari Njema
*******
Wanalibeneke watatu ambao wanajulikana kama Mapacha watatu, Michuzi Jr, Mroki Mroki na John   Bukuku leo mapema wamekutana live na Mbeya yetu Blog kwa muda mchache uliopita.
Katika mazungumzo yao mafupi wanalibeneke hao wakongwe nchini Tanzania wameipongeza Mbeya yetu Blog kwa Jitihada ambazo wameendelea kuzifanya za kupashana habari na kusisitiza ya kuwa tuendelee iendelee na kasi hiyo hiyo na kuleta habari za uhakika.
Timu nzima ya Libeneke la Mbeya yetu Blog tunapenda kuchukua Fursa hii kuwashukuru sana kwa ujio wenu na kuchukua japo Muda kidogo kuonana nasi. Tunawatakia kila laheri na mafanikio mema. Pia safari njema



No comments: