Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, March 17, 2012

MAMIA WAJITOKEZA KUPIMA MAGONJWA YA KISUKARI, SHINIKIZO LA DAMU NA UNENE - MBEYA

 Mgeni rasmi Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa  Luis Choboko, akihutubia wananchi waliojitokeza katika zoezi la kupima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya.


Mwandishi wa Mbeya yetu blog Joseph Mwaisango akiwa mojawapo ya mamia waliohudhuria kupimwa magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu


Mamia ya wakazi wa jiji la Mbeya wamejitokeza jana katika viwanja vya Ruanda Nzovwe kwa ajili ya kupima magonjwa ya Kisukari, shinikizo la damu na unene ambapo vipimo hivyo hutolewa bure na wataalamu wa afya kutoka AFPTA.

Akifungua zoezi hilo Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa  Luis Choboko amesema zoezi hilo linamanufaa makubwa kwa wananchi ambapo ametoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kupima afya zao.

Amesema zoezi hilo limelenga kupunguza msongamano wa watu kwenye vituo vya afya ambao huenda kwa ajili ya kupima zao na kwamba zaoezi hilo linatarajiwa kumalizika kesho.

Zoezi la upimaji wa afya katika viwanja vya shule ya Msingi Ruanda Nzovwe linakwenda sambamba na utoaji wa elimu ya mwananchi kujiunga na mifuko ya jamii.

Hata hivyo zoezi hili lilianzia wilaya ya Mbozi na kupata mafanikio makubwa, na kwamba zoezi litamalizika Machi 18 mwaka huu Jijini Mbeya na kuendelea katika mikoa ya Mwanza na Arusha.

 


No comments: