Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Tuesday, March 27, 2012

JIJI LA MBEYA LAZIDI KUTOA MPYA SASA WAZIBA VIRAKA VYA BARABARANI KWA KUTUMIA UDONGO

Baadhi ya mafundi wa jiji la Mbeya wakiendelea na kazi ya kuziba viraka vya barabarani kwa kutumia udongo na hii barabara haijamaliza hata miezi miwili toka viwekwe viraka vya sementi hii ni barabara muhimu sana ndiyo inayotumika kwa mabasi yote ya kwenda mikoa mbali mbali ya Tanzania

Udongo upo tayari kwenda kuwekwa kwenye mashimo ya barabara

Hapa tayari udongo umekwisha wekwa katika mashimo ya barabara angalia kwa makini picha hii utapanga wewe kuwa siku ngapi huo udongo utakuwa haupo tena kwenye shimo hilo

Hii ndiyo hali halisi 

Kweli shimo kama hili lizibwe kwa udongo?

Je tutafika?

Imbombo jilipo

Mafundi wenyewe tayari wamechoka maana mara kwa mara wanarudia barabara hii

3 comments:

Anonymous said...

Huyo Mkurugenzi wa Jiji aka Mr. Idd jiji limemshinda. Kumbe Kabwe alikuwa anauwezo wa hali ya juu!

Anonymous said...

Hii ni aibu, tena kubwa. Wako wapi viongozi? Dhamana tuliyowapa wameifanya kuwa mitaji yao. Ukoo wapi uwajibikaji? Na huyu Mh Mbuge anafanya nini? Inasikitisha sana kuona kuwa mambo haya yanafanyika katikati ya jiji sijui huko pembezoni hali ikoje. Viongozi amkeni mtimize wajibu wenu, ndio maana mpo kwenye hizo nafasi. Au mnataka hata kufanya ukarabati wa barabara za ndani waje kukarabati wafadhiri? Shame upon you! Tutakutana 2015
Mwana Mbeya

Anonymous said...

Nadhani huu ni mradi wa watu wachache wa kujiingizia pesa, utazibaje barabara kwa kutumia udongo? Viongozi wa jiji la Mbeya nadhani hawako makini na hili suala. Barabara ya kutoka stendi kuu kwenda Meta hosp. wanaziba leo mashimo baada ya wiki moja mashimo yanarudi vilevile, hawalioni hili?