Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, March 26, 2012

UJENZI WA SOKO LA MWANJELWA MBEYA UTATA MTUPU MENGI YAIBUKA


.  Mafundi waeleza ujenzi holera, Jiji wapuuza
·       Tamisemi watoa mtihani ofisi ya mkoa Mbeya
·       Polisi wafuatilia, Mbunge Sugu aguna





Site Manager -Mohamed Hasheed

SOKO jipya la kisasa la Mwanjelwa Jijini Mbeya linalojengwa baada ya kuungua mwaka 2006 halina ubora uliotarajiwa na kufadhiliwa na benki ya CRDB kwa shilingi Bilioni 14.

Uchunguzi uliofanywa na kikosi kazi chetu kwa muda wa miezi kadhaa sasa, umebaini kuwa soko hilo linanyufa zilizotokana na ujenzi uliochini ya kiwango kisha kuzibwa kwa saruji ili kuficha ubovu huo kabla ya kukabidhiwa.


Mafundi hao wamesema kuwa lawama za soko hilo kutokuwa bora zinapaswa kuwaendea waandisi wa Serikali wa Jiji la Mbeya ambao mara kwa mara wamekuwa wakifika eneo la ujenzi na kuishia ofisi za mkandarasi kisha kuondoka.

Mafundi hao ambao baadhi waliomba hifadhi ya majina yao walisema kuwa uozo huo upo tangu soko linaanza kujengwa lakini hakuna kiongozi wa Serikali ambaye amewahi kuwauliza hata mafundi kwa siri ili kujua uhalisia wa ujenzi wa soko hilo.

Kutokana na uzalendo wa mafundi hao, waliamua kumwandikia barua ya uhalisia wa soko hilo Katibu mkuu wa tawala za mikoa na Serikali za mitaa ‘’Tamisemi’’ wakieleza kuwa soko hilo halina ubora na endapo Serikali italipokea maafa yatakayotokea lawama ziwe juu ya Serikali.

Barua hizo ambazo mtadao huu unazo nakala zake, zimeeleza kuwa kama Serikali ni sikivu itafute wataalam wake na kukagua kwa kuchimbua Msingi wa Soko hilo ambapo soko hilo halina mhimili wa kuunganisha kuta (Ring bim) la kuunganisha jengo zima ili kulifanya kuwa imara.

Mafundi hao wamesma kuwa wakati wa kufanya jambo hilo wawepo kwa ajili ya ushahidi pamoja na waandishi wa habari ili kusiwepo hali ya kulindana na mazingira ya Rushwa kwa watendaji hao wa Serikali.

Kwa hisani ya G. Kalulunga

No comments: