MTU mmoja amefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili kugongana uso kwa uso maeneo ya Iwambi Jijini Mbeya ikiwemo gari la abiria aina ya Hiace iliyotokea jana usiku.
Ajali hiyo ilhusisha gari namba T200ADU aina ya Toyota Hilux iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la Isaya Saimon (34) mkazi wa Mbalizi na gari la abiria lenye namba za usajili T641ANC aina ya Toyota Hiace lililokuwa likendeshwa na Reuben Swilla (25) mkazi wa nzovwe Jijini hapa.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Advocate Nyombi alisema ajali hiyo ilitokea March 1,mwaka huu majira ya 12.30 jioni katika eneo la Iwambi ambapo gari hizo ziligongana uso kwa uso na kusababisha kifo cha dereva wa Hilux papo hapo na kujeruhi abiria 15 waliokuwa kwenye Hiace.
Alimtaja marehemu huyo kuwa ni dereva wa gari lenye namba za usajili nambaT 200 ADU ambaye ni Isaya Simon na kuongeza kuwa majeruhi 9 wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mbeya na wengine 6 walitibiwa na kuruhusiwa.
Alisema kati ya majeruhi 15 majeruhi 10 ni wanaume wakati majeruhi 5 ni wanawake walionusurika katika ajali hiyo ambapo aliongeza kuwa hali zao ni nzuri baada ya kupata matibabu.
Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari aina ya Hilux ambapo alitaka kuyapita magari mengine lakini kabla hajayapita aliona magari mengine mbele yake hivyo kuamua kuingia kwenye hiace kabla ya kupata ajali hiyo.
|
No comments:
Post a Comment