Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wimbi la wizi limeendelea kushamiri na kuchukua sura nyingne baada ya waandishi wa habari wawatu mkoani Mbeya kuibiwa mali zao na vitendea kazi.
Waandishi wa habari waliokumbwa na mkasa huu ni pamoja na mwandishi wa gazeti la Nipashe Bwana Thobias Mwanakatwe, mwandishi wetu wa mtandao huu Bwana Ezekiel Kamanga na mwandishi wa TBC Bwana Hosea Cheyo, kituo cha Mbeya ambaye majira ya saa 9 kamili usiku, eneo la Iwambi jijini Mbeya kuibiwa Desktop computer, Laptop mbili, TV inch 21, Kamera aina ya Sony, External hard disk, chaji ya kameraBroadband wire na Broadband Charger vyote vikiwa na thamani ya shilingi 3,620,000 na watu wasiofahamika.
Mbinu iliyotumika katika uporaji wa mali hizo ni kuvunja.kitasa cha mlango na kisha kuingia ndani, na upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea .
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la polisi Advocate Nyombi amesema baada ya msako mkali wamefanikiwa kuwakamata watu wawili katika kijiji cha Mlowo wilayani Mbozi, wakati wakisafirisha mali hizo kwenye gari aina ya Toyota Mark II lenye nambari za usajili T 952 ATR.
Watuhumiwa hao waliokamatwa ni pamoja na Kiongozi wa wizi huo Bwana Filbert Mbunda mkazi wa Mbalizi na dereva Christian Asajile, wakati mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Fadhili alikimbia, baada ya gari hilo kusimamishwa na Polisi wakati likielekea Tunduma.
Hata hivyo Bwana Hosea Cheyo amelishukuru jeshi la polisi kwa utendaji wao wa kazi ipasavyo, kutokana na kuijali jamii kwa kuweza kutatua kero mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama.
No comments:
Post a Comment