Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi SHAMSI VUAI NAHODHA amewahakikishia wananchi wa mbeya kuwa wizara yake kupitia jeshi la polisi limejipanga kupunguza ama kumaliza kabisa vitendo vya kihalifu vikiwemo vya upikaji nondo vilishamiri mkoani Mbeya.

NAHODHA ameyasema hayo mkoani Mbeya akizungumza na waandishi wa habari,kwamba vitendo vya kiahalifu vinavyojitokeza mara zote mkoani Mbeya vitakwisha tu ikiwa wananchi wataonesha ushirikiano wa dhati kwa askari wa jeshi la polisi kwani wanaofany avitendo hivyo wanajulikana.
Kwa taarifa zaidi na Hosea Cheyo Kwa kuwa wananchi wanaoishi, na kuingia mkoani Mbeya wamekuwa na hofu na wasiwasi dhidi ya vitendo vya kihalifu vikiwemo vya upigaji wa nondo watu vinavyotokea mara kwa mara mkoani humo,Waziri mwenye dhamana na usalama wa raia na mali zao amejitokeza mbele ya waandishi wa habari na kueleza mipango ya kufikia suluhisho.
Nahodha ambaye pamoja na mambo mengine amefika mkoani Mbeya kukagua shughuli za wizara yake,lakini amezungumzia namna ya kushughulikia suala la wahamiaji haramu na kueleza msitakabali ya watendaji wake kuwa kuna mabadiliko yanafanyika katika idara ya uhamiaji nchini.
No comments:
Post a Comment