Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Saturday, February 4, 2012

JIJI LA MBEYA LAZIDI KUWA CHAFU

Jiji la Mbeya limekua shagala bagala katika mitaa yake hali inayofanya kukosa hadhi ya kuitwa jiji kutokana na mazingira yake hayaridhishi machoni mwa watu hili ni eneo la uhindini katikati ya jiji la mbeya kwenye ofisi za mahesabu kanda ya nyanda za juu kusini ikiwa karibu na ghuba la takataka lililojaa zaidi ya wiki mbili sasa bila kuzolewa kwa taka hizo
Huku ni kata ya sinde jirani na shule ya msingi sinde eneo lote limezungukwa na takataka na kutoa harufu kali kwa wapitanjia na watoto wanaosoma shule ya msingi sinde
Hili ni eneo la kata ya manga jijini mbeya takazikiwa zimezagaa kila mahali
Hivi sasa wafanyabiashara ndogondogo wamekuwa wakijiendeshea shughuli zao mahali popote wanapojisikia na sehemu ambazo si rasmi na kufanya kuacha taka ngumu katika maeneo ya jiji na mamlaka husika kufumbia macho suala hilo na inasikitisha majalala ya kutupia taka yakiwa katikati ya barabara, kati ya nyumba na nyumba hali inayofanya uchafuzi wa mazingira na ili hali mamlaka hizo kutumia mamilioni ya fedha za walipa kodi kushughulikia taka hizo hizo
Eneo la sae
Njia panda ilomba

2 comments:

Kelkaf said...

Jiji la mbeya linazidi kukua kwa maana hasa ya idadi ya watu, shughuli za kimaendeleo na kijamii, lakini kwa upande mwingine uzalishwaji taka nao unaongezeka maradufu sasa ni vizuri pakiwepo na mikakati madhubuti kukabiliana na hali hii haiwezekani mambo yakaachwa kujiendea kienyeji enyeji tu...lakini kwani ushuru unaenda wapi kwasaabu kazi moja ya ushuru ni kuweka mazingira safi....la sivyo ushuru ufutwe au upunguzwe na watu wasimamiwe na mgambo wa jiji kuweka mazingira yao ya kazi katika hali ya usafi.

Anonymous said...

Ukisikia jijilambeya utafikiria jiji kweli kumbe ni upuuzi tu jiji gani nyumba za tope au walimnukuu vibaya aliyekuwa anazindua. Yawezekana alikuwa anazindua kijiji cha mbeya wao wakasikia jiji