MWINJILISTI Boniphace Temba amesema kuwa mpaka wa Tunduma uliopo wilayani Mbozi kati ya Tanzania na Zambia si salama kwa nchi ya Tanzania kutokana na uangalizi mdogo wa uvushaji mizigo katika mpaka huo.
Hayo ameyaeleza leo katika mkutano wake na waandishi wa habari wa mkoa wa Mbeya uliofanyika katika bustani ya Mbeya Peack Hotel iliyopo Jijini hapa.
Mwinjilisti huyo wa huduma ya Panuel Healing Ministry yenye makao yake makuu Ubungo Kibango Jijini Dar es Salaam amesema kuwa katika nchi za Afrika mashariki mpaka wa Tunduma hauna uangalizi wa usalama wa nchi hivyo umefika wakati kwa Serikali kufanya yafuatayo.
NINI KIFANYIKE Kukagua mizigo yote inayovushwa katika mpaka huo tofauti na sasa ambapo kila mtu anajivushia mizigo kadhaa bila kuulizwa, hali ambayo maadui wanaweza kuhusika kuvusha hata mabomu ambayo ni hatari kwa usalama wa nchi ya Tanzania.
Wafanyabiashara wawe mita mia moja mbali na mpaka ili kila mtu anayevuka katika mpka huo awe anaonekana na mizigo anayovuka nayo na awe anakaguliwa vema na maafisa wenye dhamana katika mpaka huo.
Ujenzi wa barabara ya Lami ya Tunduma –Sumbawanga iwe mbali na mpaka huo wakati huo huo vituo vya mafuta vijengwe mbali na mpaka kwa ajili ya usalama wa wananchi wanaoishi na kufanya biashara katika mpka huo wa Tunduma.
USALAMA TUNDUMA Sanjari na hayo alitanabaisha kuwa Tanzania katika mpaka huo inatia aibu kwasababu ya kushindwa kuuweka katika hali ya kiusalama na sasa biashara kubwa inayofanyika na baadhi ya wananchi ni kuwavusha waamiaji haramu na kujipatia kipato jambo ambalo ni hatari kwa usalama wan chi.
‘’Kutokana na waliopewa dhamana kushindwa kufanya kazi ipasavyo kutokana na mazingira yalivyo, kwa sasa baadhi ya wananchi wanafanya biashara ya kuwavusha wahamiaji haramu bila kujua kuwa wamebeba nini jambo ambalom endapo Serikali na Bunge watapuuzia kuna siku Tanzania Amani na utulivu vitatoweka’’ alisema Mwinjilisti Temba.
Aliweka wazi kuwa katika mpaka huo wa Tunduma, watu wanaohusika katika usafirishaji wa wa wahamiaji haramu ni wale ambao walikuwa wanahusika na usafirishaji wa Wasomali na sasa wanasafirisha wahamiaji kutoka nchi za Ruanda na Burundi kuelekea Afrika kusini.
UCHUMI. Akielezea changamoto za uchumi kutokana na mpaka huo wa Tunduma kuwa wa kienyeji kuliko mipaka yote ya Tanzania, amesema uchunguzi alioufanya unaonyesha kuwa kila siku iendayo kwa Mungu Tanzania inapoteza Dola 50,000 mpaka dola 100,000 za kimarekani kwa siku kutokana na miundombinu kutowekwa sawa.
Alisema licha ya mpaka huo kukaa shaghala baghala na kupoteza mapato ya nchi, lawama zinapaswa kuelekezwa kwa Wataalam wa masuala ya uchumi ambao wengi wao baada ya kuwa na madaraka wamepofushwa.
WANANCHI KUTOTII SHERIA
Ametanabaisha kuwa asilimia 60-75 ya wananchi wa Tanzania hawatii sheria za nchi jambo ambalo viongozi wengi wa siasa huingili ma kuwashawishi wafuasi wao hasa vijana kutaka kuandamana kisha wapate umaarufu b ila kujali uzalendo kwa nchi.
MCHAKATO WA KATIBA MPYA.
Mwinjilisti huyo amesema kuwa katika midahalo inayoendelea nchini juu ya mabadiliko ya Katiba Mpya, amependekeza kuwa dawa sahihi ya ajali nchini kwanza ni kutii sheria pasipo kushurutishwa, kuboresha ujenzi wa barabara kuu kwa kuzitanua zaidi na kuruhusu mabasi kufanya safari usiku kwasababu nchi inaonekana kuwa ni nchi yenye Amani na Utilivu.
Amesema amelazimika kutoa ushauri huo kwa Serikali kutokana na uzalendo wake kwa nchi yetu ya Tanzania kwasababu ushauri wa namna kama hiyo aliutoa hivvi karibuni kwa Rais wa DRC Joseph Kabila kwa ajili ya umuhimu wa Amani na kutotumia nguvu inayozidi ya Dola. |
No comments:
Post a Comment