Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, January 2, 2012

HOT NUUZ!! SAKATA LA KUTENGENEZA BARA BARA YA LAMI KWA KUTUMIA CEMENT: MKURUGENZI WA JIJI ASEMA BARABARA IMETENGEWA MILIONI 400 KWA AJILI YA UKARABATI.

Hii ndio Bara bara ya Mbalizi Road Maeneo ya Hospitali ya wazazi Meta Jijini Mbeya, Ikiwa imezibwa viraka kwa kutumia Cement 
 Baadhi ya Viraka vikiwa vimezibwa
 Mafundi wakiwa bize wanahangaika kuziba viraka hivyo

 Wafanya kazi wa Jiji wakiendelea kukoroga zege tayari kupeleka kuziba viraka katika bara bara ya lami
 Shughuri ya kuziba viraka kwa kutumia cement imekamilika, Inasubiri kukauka magari yaanze kupita


 Mafundi wakiendelea kuziba mashimo ya Bara bara kwa Kutumia Cement
Mkurugenzi wa Jiji La Mbeya akiongea na waandishi wahabari
Mmoja wa Waheshimiwa Madiwani akihoji juu ya uzibaji wa viraka vya bara barani, na kusema kama vinafaa akawambie wananchi nao waanze kuziba bara bara hizo kwa kutumia Cement

****************************
Ukarabati wa barabara wa aina yake tofauti na utaalamu yakinifu, Mkurugenzi wa Jiji Bwana Juma Idd amesema hatua hii ni ya muda kwani barabara hiyo imetengewa jumla ya shilingi milioni 400, ambapo Mkandarasi amekwisha patikana na shughuli za ukarabati zitaanza mara baada ya msimu wa mvua kuisha.

 Mtandao huu umeshuhudia ukarabati ukiendelea eneo la Kanisa la Sabato barabara ya Mbalizi kutokea Meta jijini hapa ambapo Saruji imetumika kuziba viraka katika barabara hiyo, badala ya kutumia Lami ambapo huigharimu serikali kutokana na viraka hivyo kubanduka baada ya muda mfupi.

Hata hivyo mwaka uliopita barabara hiyo iligharimu shilingi milioni 57, licha ya Mkurugenzi huyo kutokuwa tarai kutaja kiasi cha gharama zilizotumika kukarabati barabara hiyo kwa mwaka huu na kudai kuwa ni kiasi kidogo kimetumika.

Wakati huo huo Baraza la madiwani wa Kata zote 36 za jiji la Mbeya limelalamika kuwepo kwa miundombinu mibovu ya barabara hizo na utendaji mbovu wa makandarasi ambao huzijenga barabara hizo licha ya kupewa pesa nyingi.


No comments: