Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Friday, December 16, 2011

MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA YATANGAZWA



WASICHANA wameongoza katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa ajili ya  kujiunga na kidato cha kwanza kutokana na  mtihani uliofanyika Septemba mwaka huu mkoani Mbeya, huku mwanafunzi wa shule ya msingi  ya Airport ya jijini Mbeya Vaileth Sanga akishikilia usukukani kwa kupata alama 225.
Mwanafunzi mwingine  aliyepata alama 225 ni John Mwaipopo kutoka katika shule ya binafsi ya UWATA  ambapo idadi ya wasichana waliochaguliwa kujiunga na sekondari ni 22,104.
Akitangaza matokeo hayo Ofisa elimu wa mkoa wa Mbeya Bw. Juma Kaponda alisema kuwa idadi hiyo ya wasichana iko juu dhidi ya wavulana ambao ni 21,136 kati ya watahiniwa 78,667 ambayo ni sawa na wasichana 41,226 na wavulana 37,240.
Alisema kuwa idadi hiyo ya ufaulu ni sawa na asilimia 55 ambapo jumla ya waliochaguliwa kujiunga na sekondari za bweni ni  262 ambao ni wavulana 176 na wasichana  86 ilhali waliochaguliwa katika shule za kutwa ni 32,371 ambao kati yao ni wasichani 16,389 na wavulana ni 15,982.

Aidha Bw. Kaponda alisema kuwa jumla ya wanafunzi 10,607 wameachwa katika uteuzi wa awamu ya kwanza kutokana na uhabwa vyumba 242 vya madarasa na kuwa uteuzi huo wa awamu ya pili utafanyika mara baada ya kukamilika kwa vyumba hivyo na kwamba kati yao wasichana ni 5,629 na wavulana ni 4,978.
Alisema kuwa waliochaguliwa vipaji maalumu ni  72 ambao kati yao ni wavulana 38 na wasichana 34 ambapo 100 wamechaguliwa kujiunga na shule za ufundi stadi wakiwemo wavulana 73 na wasichana 7 ambapo waliojiunga na sekondari za bweni kwa shule za kawaida ni 110 kati yao wasichana 45 na wavulana 65,
Pia Bw. Kaponda alisema kuwa watahiniwa wenye ulemavu walikuwa ni 78 ambapo kati yao waliochaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ni 39.
Bw. Kponda liitaja shule iliyoongoza kwa kufanya vizuri kuwa ni shule ya Msingi Bulyaga iliyopo wilayani Rungwe na shule ya mwisho ni ya Masanyita iliyopo wilayani Mbozi huku wanafunzi saba wakiambulia sifuri katika mtihani  huo.



No comments: