MKOANI MBEYA WAKALA wa Barabara nchini (Tanroads) wameamka kwa kuanza kuwatimua makandarasi wa makampuni ya nje ya nchi ambao hawana sifa za kusimamia ujenzi wa Barabara nchini wakati ambao wameitia hasara Serikali kwa zaidi ya miaka mitatu.
Tanroads wameanza kuchukua hatua hizo kwa kampuni ya Nicholas O’Dwyer & Company Ltd ya Uingereza kwa kumtimua aliyekuwa anajiita injinia Ciaran Cleere.
Kampuni hiyo inatuhumiwa pia kusababisha kukwama kwa ujenzi wa Barabaya ya Mbeya – Lwanjiro yenye urefu wa Kilomita 36 iliyopo mkoani Mbeya iliyokuwa imesainiwa mkataba wa Bilioni 40.
Kutimuliwa kwa Mkandarasi huyo ambaye aliajiriwa nchini kama mhandisi mshauri, kumebainika baada ya barua ya wakala wa Barabara nchini Tanroads ya Novemba 25, mwaka huu yenye kumbukumbu namba TRD/HQ/11/129/01/12 iliyosainiwa na Mhandisi Chrispianus B. Ako ikiiendea kampuni hiyo ya Nicholas O’Dwyer ambayo Gazeti hili linayo nakala yake.
Barua hiyo ambayo imeambatanishwa hapo juu inaeleza kuwa, haimtaki kumwona katika miradi yeyote hasa mhandisi huyo hasa katika ujenzi wa barabara ya Korogwe- Mkumbara yenye urefu wa kilomita 76 na barabra ya Mkubara-Same yenye urefu wa kilomita 96.
Mkandarasi huyo katika miradi hiyo aliajiliwa kama mhandisi mshauri katika mkataba wenye kumbukumbu namba TRD/HQ/ 11/129/10.
Tanroad katika barua hiyo inasema udhaifu wa Mhandisi huyo ulianza kuonekana na kujidhihilisha katika mradi wa Barabara ya Mbeya-Lwanjilo iliyopo mkoani Mbeya ambao aliingiza Serikali hasara kwa kuidanganya kuwa Mkadarasi aliyekuwa akijenga barabara hiyo kampuni ya Kundam Singh Construction Ltd hakuwa na uwezo.
Udanganyifu huo ulipelekea kusimama kwa mradi huo ambao mpaka sasa haujakamilika licha ya kuajiri mkandarasi mwingine kwa gharama kubwa huku Tanroad ikishindwa kesi ya Msingi kati yake na mkandarasi Kundan Singh anayejenga kiwanja cha ndege cha Songwe.
Kutokana na mwandisi huyo mshauri kutokuwa mkweli na kusababisha miradi kadhaa kusimama, imeelezwa kuwa amemponza pia aliyekuwa Meneja wa Tanroad mkoa wa Mbeya Lucian Kileo ambaye katika mabadiliko ya mameneja yaliyotokea hivi karibuni kote nchini ameenguliwa na kusubiri kupangiwa kazi nyingine.
Mhandisi mshauri huyo kampuni ya Nicholas O’Dwyer & Company Ltd aliwahi kulalamikiwa wakati ujenzi wa barabara ya Mbeya - Chunya kuwa anamainjiia wasio na sifa lakini kaendelea kulindwa mpaka hivi karibuni ilipobainika kuwa hana uwezo. Awali bodi ya usajiri wa mainjinia nchini (Engineers Registration Boad) hivi karibuni ilimkataza injinia Duncan White wa kampuni hiyo ya Nicholas O’Dwyer & Company Ltd kujihusisha na kazi ya uinjinia hapa nchini na kusababisha Tanroads kusikitika.
Barua kutoka kwenye bodi hiyo iliandikwa Mei 3 mwaka huu na kusainiwa na msajiri, Injinia Steven Mlote na kueleza kuwa kutokana na maombi aliyotuma Duncan White ili apewe kibali kama Injinia yalikataliwa kwa kifungu cha sheria namba 15 ya mwaka 1997 ambayo ilifanyiwa marekebisho kifungu cha 6 cha usajiri wa mainjinia na sheria namba 24 ya mwaka 2007.
Barua hiyo yenye kumbu kumbu namba ERB/TPE/934/6 imesambazwa nakala zake kwa Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Nicholas O’Dwyer $ Co. Ltd Mbeya, Mkurugenzi wa idara ya Uhamihaji Dar es Salaam na kupelekwa ofisi ya Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) makao makuu.
Ijinia huyo ndiye aliyekuwa anasimamia ujenzi wa madaraja yaliyopo Barabara ya Mbeya-Lwanjiro na ndiye alikuwa tarajio la kusimamia madaraja manne yaliyopo katika Barabara ya Lwanjiro- Chunya ambayo ni daraja la Isewe,Chalangwa, Itumba 1 na Itumba 2.
|
No comments:
Post a Comment