Social Icons

Sikiliza Tone Radio Live Hapa, na Tembelea Website yetu www.toneradiotz.com

bre

Monday, December 19, 2011

ASKARI POLISI MBEYA WADAIWA KUHUSISHWA NA WIZI WA GARI


RPC MBEYA ADVOCATE NYOMBI

GARI KAMA HILI AINA YA TOYOTA IPSUM NDILO LINALODAIWA KUIBIWA KWA KUSHIRIKIANA NA ASKARI POLISI MBEYA



ASKARI polisi wanne wa wilayani Mbozi mkoani Mbeya ambao majina na namba zao tunazihifadhi wanadaiwa kushiriki katika kula njama ya kutorosha gari la wizi kwa kuhongwa fedha zaidi ya shilingi milioni 2.
Gari hilo ambalo awali lilikuwa na namba za IT likiwa linasafirishwa kwenda nje ya nchi lilitua mikononi mwa askari hao ambao ni askari wa usalama barabarani askari wawili wa kike wenye namba za WP 44..,WP47..,F49..PC.. na F 47..PC...ambao wanahojiwa kwa tuhuma za kula njama ya kutorosha gari hilo.Inadaiwa kuwa gari hilo liliibiwa katika bandari ya Dar es salaam Novemba mwaka huu na kusafirishwa hadi Tunduma ambapo baadaye likiwa na namba za bandia lilianza safari ya kurejeshwa jijini Dar es salaam kupitia jijini Mbeya kwa njia za panya huku likiwa na watu wawili mmoja wao akiwa dereva.
Gari hilo lilifika katika mji mdogo wa Mlowo na kutiliwa mashaka na askari usalama barabarani wa kike WP 50… PC …na WP-44... PC … ambao nao waliwashirikisha F-49.. PC … na F 47.. PC...
Imedaiwa kuwa mara baada ya mahojiano watu hao walikiri kuwa gari hilo ni la wizi na kuwaomba askari hao wachukue sh.500,000/- ili wawaachie lakini askari hao inadaiwa waliomba wapewe kiasi cha milioni 2 ambazo hata hivyo hawakuwa nazo na kuwaomba askari hao walete siku inayofuata huku gari likiwa mikononi mwa mmoja wa askari hao.Imedaiwa kuwa gari hilo lilichukuliwa na kwenda kufichwa askari mmoja wa kike eneo la Mlowo hadi siku waliyoahidiana.
Imeelezwa kuwa siku ya ahadi jamaa hao walipeleka kiasi hicho cha fedha kwa askari hao na kuwaomba askari hao wawasaidie kuwasindikiza hadi nje ya mkoa ili wasisumbuliwe na askari wengine barabarani.
Inadaiwa kuwa askari wawili walibaki Mlowo na askari wa kike wawili walilisindikiza gari huku mmoja wao akiliendesha na wenyewe wakiwa wamekaa nyuma ya gari.Taarifa zaidi zinadai kuwa wakiwa safarini kuli ‘save’ gari hilo walikutana na vigingi katika kijiji cha Ruanda ambapo askari wa eneo hilo walipewa tip kuwa gari hilo ni dili hivyo lazima upite mgawo.
Hata hivyo askari hao waliposimamisha gari hilo hawakuweza kusimama ndipo wakaanza kufukuzana askari kwa askari hadi eneo la Senjele katika daraja la treni na kuanza kuzozana wakitaka wakitaka upite mgawo wa mshiko huo.
Imedaiwa kuwa askari hao wapya waliomba wapewe sh.milioni 2 zingine ambapo alikataliwa na watu hao ambao walidai walibakiwa na sh.milioni 1 tu.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kushindwa kuafikikiana mmoja wa askari hao alipiga simu ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya  ambapo walitumwa askari wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu kwenda eneo la tukio.  
Imedaiwa  kuwa baada ya kushindwa kuafikiana askari hao wa kike waliondoka kwa gari binafsi la mmoja wao na kurudi Mlowo ambapo huku nyuma askari kutoka jijini Mbeya walifika na kuwakuta wenzao wa Vwawa wakiwa na watu hao ambapo walimchukua mmoja wao aliyefahamika kwa jina moja la Twalib huku wale wa Vwawa wakiondoka na mwingine aliyedaiwa kuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Hata hivyo katika hali ya kushangaza baada ya kufika Kituo Kikuu Cha Polisi cha  Jijini Mbeya na Twalib mtu mwingine aliyekuwa na trafiki wa Vwawa  hakuonekana hali ambayo imeongeza wasiwasi wa tukio hilo.

Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa askari hao wa kike kati ya askari wanaodaiwa kuhusika na tukio hilo alisema kuwa kwa wakati huo anatoka kanisani na kuwa hawezi kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa kuwa msemaji wa polisi ni Kamanda wa polisi mkoa.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Advocate Nyombi amekiri kutokea kwa tukio hilo hata hivyo amesema kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Twalib Soud anashikiliwa kwa kuhusika na wizi wa gari hilo aina ya Toyota IPsum ambalo limewekwa namba za kubandika T 173BKT.
Kamanda Nyombi alisema kuwa taarifa zilizopo askari Trafiki wilayani Mbozi ndio waliolikamata gari hilo baada ya kulitilia mashaka na kwamba uchunguzi zaidi unaendelea.

No comments: