Mchungaji wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya Anyandwile Kajange, akila chakula na watoto yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi ikiwa ni ishara ya upendo kwa watoto hao, baada ya kanisa hilo kutoa nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Bi Beatrice Mwinuka mjumbe wa Halmashauri kuu ya Jimbo ya kanisa la Moravian Tanzamia.
Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu na hatarishi, wakisubiria kwa hamu zoezi la ugawaji wa nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane, ambapo Mgeni rasmi alikuwa Bi Beatrice Mwinuka mjumbe wa Halmashauri kuu ya Jimbo ya kanisa la Moravian Tanzamia.
Mgeni rasmi wa ugawaji wa zawadi kwa watoto yatima, wajane na wanaoishi katika mazingira hatarishi Bi Beatrice Mwinuka(kushoto), pamoja na Mchungaji wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya Anyandwile Kajange wakiwa wameketi kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa zawadi zikiwemo nguo za sikukuu zenye thamani ya shilingi laki nane
Kushoto ni mtoto Julius Sikaonga mwenye umri wa miaka 2, ambaye amekuwa akilelewa na bibi huyo Bi Lucia Minga ambaye alimokota mtoto huyo Januari 18, mwaka 2009 katika mtaa wa majengo mji mdogo wa Tunduma ambapo mpaka hivi sasa mtoto huyo anaendelwea vizuri, hivyo ni mfano kwa wananchi wengine kuwa na roho yahuruma na kusaidiana katika jamii.
Mgeni rasmi Bi Beatrice Mwinuka akigawa zawadi kwa mmoja kati ya wajane walionufaika na msaada wa Kanisa la Moravian Ushirika wa Mwaka Tunduma mkoani Mbeya.
Mchungaji Anyandwile Kajange akishuhudia zawadi zikitolewa kwa wajane, watoto yatina na waishio katika mazingira hatarishi.
Watoto hao wakila chakula kwa pamoja, licha ya kushindwa kujieleza majina yao kutokana na umri. Watoto hawa walifiwa na wazazi wote wawili hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment