Pikipiki nambari T 156 BRE iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Abinel Maliva iligonga kwa nyuma gari nambari T 605 BBK aina ya Toyota RAV4 iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Juma Abubakari katika eneo la Esso jijini Mbeya.
*****
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya
Wananchi wa kijiji cha Ilongo, wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya walifunga barabara kuu ya Mbeya - Iringa jana kwa muda wa masaa mawili, baada ya mkazi mmoja wa kijiji hicho kugongwa na gari aina ya roli na kisha kupoteza maisha.
Marehemu aliyefahamika kwa jina la Magreth Tito (19), ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mapo Ruiwa, majira ya saa 6 mchana baada ya kugongwa na roli hilo lenye nambari za usajili T. 204 BNC lililokuwa na tela lenye nambari T 319 AYK ambalo dereva wake hakuweza kufahamika kutokana na roli hilo kutosimama baada ya kusababisha ajali hiyo.
Baada ya ajali hiyo kutokea wananchi wa kijiji hicho walitoa taarifa kituo cha polisi, lakini kutokana na Jeshi la polisi kuchelewa kufika wananchi hao walizua magari kutoendelea na safari baada ya kupanga magogo na mawe barabarani kwa lengo la kuzuia mwili wa marehemu usipondwe na magari mengine.
Kumekuwepo na ajali nyingi eneo hilo kutokana na msongamano wa watu wengi eneo hilo kwani limekuwa likitumika kama kituo cha mabasi makubwa na madogo na hivyo kuiomba Serikali kuweka matuta, licha ya kuwepo kwa vibao vyenye ishara ya kupunguza mwendokasi lakini madereva wamekuwa wakipuuza.
Hata hivyo baada ya dereva huyo kukimbia, alilitelekeza roli hilo katika kituo cha mafuta kilichopo Igurusi wilayani humo, ambapo chanzo kimetanjwa kuwa mwendokasi wa gari hilo.
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na hivyo jeshi lake kuweza kudhibiti hali hiyo ya wananchi kufunga barabara na hivyo kuruhusu magari kuendelea na safari majira ya saa nane mchana.
Ameongeza kuwa pikipiki nambari T 156 BRE iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Abinel Maliva iligonga kwa nyuma gari nambari T 605 BBK aina ya Toyota RAV4 iliyokuwa ikiendeshwa na Bwana Juma Abubakari katika eneo la Esso jijini Mbeya.
Dereva huyo wa pikipiki alikuwa katika hali ya mwendokasi alishindwa kuimudu pikipiki na hivyo kugonga kwa nyumba kioo na kupasuka ambapo alijeruhiwa kichwani na puani hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa jijini hapa mpaka mauti yalipomfika.
No comments:
Post a Comment