Mbunge  wa mstaafu wa Jimbo la Ileje ambaye pia ni Kamanda wa UVCCM wilaya ya  Ileje Mheshimiwa Gideon Cheyo amesema kiongozi ataheshimiwa kwa matendo  yake, wala si kwa heshima au cheo chake bali ni katika  hali ya  kuwajibika kwa wananchi waliompa dhamana ya Uongozi.
 Katibu  wa UVCCM mkoani Mbeya Bwana Ramadhani Kizinga amewataka makatibu wa  UVCCM wa wilaya zote mkoani Mbeya kufanya kazi kwa bidii na maadili na  kanuni ya Chama cha Mapinduzi (CCM), vinginevyo watawajibishwa kwa  mujibu wa sheria.
Kamanda  wa UVCCM mkoa wa Mbeya Dokta Stephen Mwakajumilo, amewataka vijana wa  UVCCM kutotumiwa kama watu wa kuwawezesha watu wasiokuwa na sifa kuingia  madarakani na hivyo kutosimamia sera madhubuti za Chama Cha Mapinduzi  na serikali yake.
Baadhi  ya wanachama Baraza la Vijana UVCCM wilaya ya Ileje mkoani Mbeya  wakimsikiliza Kamanda wa UVCCM mkoa wa Mbeya Dr. Stephen Mwakajumilo  katika Ukumbi wa CCM wilayani humo.
No comments:
Post a Comment