Na Ezekiel Kamanga, Mbozi.
Bwana Iman Labi Kalinga (22) mkazi wa kijiji cha Mpanda, kata ya Nyimbili wilayani Mbozi mkoani Mbeya anatuhumiwa kumuua mdogo wake kisha kunyofoa baadhi ya viungo baada ya kuahidiwa kupewa pikipiki yenye thamani ya shilingi milioni moja na mfanyabiashara jina tunalo.
Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi jioni, kijijini hapo ambapo mtuhumiwa Bwana Imani Kalinga alimuua Bwana Heron Yuen Kalinga (17), kisha kuondoa baadhi ya viongo vyake ukiwemo moyo, ulimi na sehemu za siri.
Kwa upande Mtendaji wa kijiji cha Mpanda Bwana Nelbert Shonza amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kwamba baadhi ya watu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi hivi sasa wilayani Mbozi kwa kuhusika na tukio hilo akiwemo mfanyabiashara maarufu wa eneo la Ilolo wilayani humo.
Hata hivyo kutokana na tukio hilo mtuhumiwa Bwana Imani Mwakalinga alinusurika kupingwa na wananchi wenye hasira kali ambapo aliokolewa na Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Nelbert na kwamba imesaidia kwa mchango mkubwa kuwapata watu wengine walioshiriki katika mauaji hayo.
Naye Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Advocate Nyombi amesema Mkuu wa upelelezi mkoa Anacletus Malindisa ambaye alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi atatolea taarifa juu ya tukio hilo.

No comments:
Post a Comment